SABABU YA KWANZA
SABABU YA PILI
SOMA: MWANZO 4:11-12
Basi sasa umelaaniwa wewe katika ardhi , iliyofumbua kichwa chake
ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako
Utakapoilima ardhi haitakupa mazao
yake ; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikoa duniani.
Huwezi kutulia mahali,unajaribu
kujenga hapa pana kataa unajaribu kukaa hapa panakataa lakini haujajua ya
kwamba unapata shida kwa sababu ya shida
iliyopo kwenye ardhi…uharibifu uliotokea kwenye ardhi unakufanya kutotulia …Biblia isinge semesha masuala haya
ingekua shida sana
SABABU YA TATU
SOMA: 2 NYAKATI 7:12-14
Bwana akamtokaea Sulemani usiku,
akamwambia , nimesikis ulivyo omba na mahalia hapa nimejichagulia kuwa nyumba
yangu ya dhabihu .
Nikizifunga mbingu isiwe mvua ,
tena nikiamuru nzige kula nchi au nikiwapelekea watu wangu tauni;
nNchi
ni mipaka yenye ardhi halali na taifa ni kundi la watu waliokubalia kuwa na
mfumo wa uongozi wa kuwaunga pamoja
Ndio
maaana kweny Biblia familia inaweza kuwa taifa ..na watu wengi sana wengi sana
wanapotaka kuliombea taifa …
Biblia inasema .. *” nikizifunga
mbingu isiwe mvua“* kama ukosekanaji wa
mvua katiaka eneo lenu unatokana na
kufungwa kwa mbingu … maana yake mbinu inaweza na mawingu lakini mvua isinyeshe
Biblia inasema tena … *” tena
nikiamuru nzige kula nchi”*……maana yake wadudu waharibifu watakuja kuharibu
kuharibu vitu vilivyopo kwenye ardhi.
Unaweza kuutumia huu mstari kuombea
taifa ni sawa kabisa lakini uwe na uhakika kuna vitu havitatokea , hauta ona
matokeo yake …wewew utakuwa una tafuta uponyaji wa watu lakini Mungu anaangalia
uponyaji wa Ardhi, mnatazama vitu viwili tofauti….ni kama Mungu anasema umpokee
kiwanja cha ndege cha Iringa wewe unaenda kumpokea Dar.
Mungu anapo weka mstari wa ahadi cheki mwiso wake. Itafsiri Biblia jinsi ilivyo, Cheki Mungu ameahidi nini lasivyo utapata shida sana .
SOMA: YEREMIA 22:29-30
Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neon
la Bwana
Bwana asema hivi, Andikeni habri za
mtu huyu kwamba hana watoto , kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zote ; maana
hapana mtu katika uzao wake akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi na kutawala
tena katika Yuda.
Wakati adhabu inatolewa kwa mtu huyu alikuwa bado hana watoto , kwa hiyo kumbukumbu kwenye ardhi ni kwamba ni kwamba hana moto na kumbukumbu zina sema kwamba hata atakapopata watoto hata fanikiwa .
SOMA: MWANZO 28: 10-20
10 Yakobo akatoka Beer-sheba , kwenda harani 11 Akafika mahali
Fulani akalala huko usiku kucha , maana jua lilikuwa limekuchwa ,akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake , akalala
usingizi palapale 12 Akaota ndoto, na tazama ngazi imesimamishwa juu ya nchi,
na ncha yake yafika mbinguni .Tena tazama malaika wanapanda na kushuaka juu ya yake 13 Na
tazama Bwana amesimama juu yake , akasema mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahim baba
yako na Mungu wa Isaka , nch hii uilalayo ntakupa wewe na uzao wako
Nimeona wengine wamekuwa wakiteseka
kutokana na mahali walipo lala wakiwa shuleni(bording)
SABABU YA SITA
SOMA: 2 SAMWELI 21:1
Kulikuwa na njaa siku za daudi muda wa miaka mitatu , mwaka hadi mwaka naye Daudi akautafuta uso wa Bwana , Bwana
akasema ni kwa ajili ya Saul, na nyumba yake yenye damu kwa kuwa aliwaua hao wagibeoni.
Ukisoma ule mstari wa 14.. unaona
Mungu anaiponya ardhi ;
Kwa hiyo Mungu alikuwa anaponya ili
kumsaidia daudi kwenye kipindi chake ambapo kulikuwa na njaa kusiwe na njaa na
kuwe na chakula …. Biblia inasema ….. alipata kibali ikaachiliwa Baraka, Baraka
iliondolewa makusudi kabisa
SOMA: UFUNUO 12:12- 15
Kwa hiyo shangilieni; enyi mbigu
,nanyi mkaao humo ole wan chi na bahari ! kwa maana Yule ameshuka kwenu kwenye
ghadhabu nyingi akijua ya kuwa ana mda mchache tu
Na Yule joka alipoona ametupwa
katika nchi alimwudhi mwanamke Yule aliyezaa
mtoto mwanaume
Mwanamke Yule akapewa mabawa mawili
ya tai Yule mkubwa ili aruke aende zake nyikani , hata mahali pake, hapo
alishwapo kwa wakati na nyakati na nusu ya wakati mbali na nyoka huyo,
Nyoka akatoa katika kinywa
chakenyuma ya huyo mwanamke maji kama moto amfanye kuchukuliwa na mto ule.
SOMA: YOELI 7:9-13
Utaombaje ikiwa hali ya kiroho ya ardhi imesababisha sadaka zizuiliwe kutolewa kanisani. Wachungaji wapo kanisani wao wanamwomba Mungu awasaidie watu watoe sadaka sawasawa Mungu ana sema hapana shida sio kutoa sadaka sawasawa sadaka zilikuz zinakuja ni mimi niliyezizuia … badala ya kuombea wakristo ombea hali ya ardhi ya nyumbani kwao ..ikishapona ardhi swala la kutoa sadaka litakuwa rahisi sana
SABABU YA TISA
SOMA: KUMBUKUMBU LA TORATI 8 7-12
Nilitaka uone lile neno kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake ina mahusiano na Baraka za Mungu juu ya watu walioingizwa kwenye nchi au kwenye mipaka halali ya umiliki. Ndio maana kati ya adhabu mojawapo inaifikia nchi ni miji kubomolewa au kukosa wakazi, kuwa ukiwa , kuwa mahame;…….laana aliyoilaani Yesu miji ya Bethsaida katiaka nchi ya Israeli tumepita kule ni magofu mpaka leo.
Biblia inazungumza Mungu akirudia eneo anawapa na uwezo watu wliorudi kujenga pale kwa upya , wanajenga na wana kaa nadni yake . Na wale ambao Mungu aliwabbarikia na wakajenga halafu wakamkorofisha Mungu, Biblia inasema watajenga na wasikae ndani.
*Pia kuna uhusiano gani ulioppo kati ya ardhi na cheo….. kosa la kiti na kosa la mtu aliyekaa kwenye kiti …. Kosa la kiti adhabu yake atapata kila mtu atakayekaa kwenye kiti… kwa hiyo kumfukuza kwa jinsi ya mwili kwa sababu amekosea haitutui tatizo la kiroho lililofanya akakose kwa hiyo mtu mwingine atakayekuja atajikwaa palepale ….kwa sababu tatizo sio mtu ni kiti.* Ndicho kilichompoza Daudi tataizo halikuwa kwake wala Sauli….tatizo ni maamuzi ya Sauli alipokuwa amekaa kwenye kiti. Sio kwamba daudi alirithi kiti alirithi na adhabu iliyokuwa kwenye kiti.
Kati ya jambo moja ambalo watu wamepata shida ni roho ya kukataliwa …ambayo ilimsumbua pia na Kaini……unakatataliwa na ngugu zako , unakataliwa na watoto wako , unakataliwa na mume au mke …. Kwa wachungaji unakataliwa na waumini bila maelezo. …. Unajiuliza ni kwa nini …. Ni ardhi iliyobeba roho ya kukataliwa…. Ndio maana kuna ardhi zinazo kataa wenyeji wasijenge kwao…unakuta wageni wana nyumba nzuri tu na sio kwamba wenyeji hawana hela.
MUNGU AKUBARIKI SANA
MAHITAJI TUMA HAPA
SIMU: +255762756542
WATSAP: +255762756542
E-MAIL: mchungajilaurent@gmail.com
youtube:"Upenyo Wa Mungu Tv"
0 Comments