UTANGULIZI
Bwana YESU asifiwe mpendwa wa madhabahu hii, Ninakupenda.
Karibu tujifunze neno la MUNGU muda na wakati kama huu. Leo tunaenda kujifunza
somo juu ya “Mafanikio ya kiroho na kimwili”, kupitia mbinu mbalimbali ambazo
Mimi napenda kuziita ” SAYANSI YA MAFANIKIO”.
MAANA YA MAFANIKIO
Kama wasafiri hapa duniani, binadamu tumekuwa tukipigana na
kujitahidi kwamba tupate MAFANIKIO ili siku pale parapanda litakapolia basi mtu
aweze kuondoka na kuacha alama, kwamba alikuwa amefanikiwa au hakufanikiwa.
Je, MAFANIKIO katika maisha ya binadamu ninini?, yanakuwa
defined vipi?, Ni yapi yanatufanya tuseme Fulani kafanikiwa kimaisha?, Je,kuwa
na Mali nyingi, magari,nyumba, pesa n.k ni MAFANIKIO katika maisha?, Je, kuwa
na kazi nzuri yenye mshahara mzuri ni mafanikio?, Je,kulishika neno la Mungu na
kumwamini ni MAFANIKIO katika maisha?
MAFANIKIO-NI ILE HALI YA KUJIHISI VIZURI KUTOKANA NA
KUISHINDA AU KUZISHINDA CHANGAMOTO ZILIZOPO NA ZILE ZINAZOJIINUA KATIKA MAISHA;
MSINGI WA SOMO HILI
NI HUU
a) Kufanikiwa kwa kusudi la Mungu kunategemea namna
unavyotumia FURSA anazoleta Mungu maishani mwako (MAFANIKIO ya kiroho).
b) Kufanikiwa kwa maisha yako binafsi kunategemea namna
unavyotumia FURSA anazoleta Mungu maishani mwako. Ni Mara ngapi Roho mtakatifu
amekufunulia siri ya mafanikio halafu hukutii?.
Zaburi 133:1 “Tazama jinsi ilivyovema na kupendeza ndugu
wakae pamoja kwa umoja”.
MUNGU AKUBARIKI SANA
ENDELEA KUFUATILIA
MAOMBI NA MAOMBEZI
MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
0762756542
WATSAP: 0762756542
0 Comments