Follow us

Jinsi Ya Kutoka Kwenye Vifungo Vya Giza.

Tangazo

                                

MCHUNGAJI LAURENT MPOMA

Kifungo cha kipepo

Kifungo cha kipepo ni adhabu ya mtu kuwekwa jela kipepo na mawakala wa shetani.

Wako watu wengi tu wanateswa na vifungo vya giza katika maisha yao, wengine wanatamani watoke katika vifungo hivyo lakini imeshindikana maana wanaenenda kimwili na sio kiroho.

Zaburi 142:7 "Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki watanizunguka, Kwa kuwa Wewe unanikirimu."

Jambo la kwanza kabisa nataka kukuambia ni kwamba Bwana YESU alikuja ili kuzivunja na kuziharibu kazi zote za shetani vikiwemo vifungo vya kipepo.

1 Yohana 3:8b "Kwa kusudi hili Mwana wa MUNGU alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi."

VIFUNGO HIVYO VYA GIZA.

1. Kuibiwa ufahamu kipepo ili ulitumikie kusudi la shetani na sio la MUNGU.

Kuna watu wengi fahamu zao zimefungwa kipepo kiasi kwamba wanalitumikia kusudi la shetani na sio la MUNGU, Leo kwa njia ya maombi yako katika jina la YESU KRISTO hakikisha unakiharibu kifungo hicho cha giza kilichokufunga ufahamu.

2 Wakorintho 10:4-5 " (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)

 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya MUNGU; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii KRISTO;"

2. Kutekwa na nguvu za giza.

Baadhi ya dalili ya mtu aliye katika kifungu cha kutekwa na nguvu za giza ni kuonewa sana na majini au wachawi kwa sababu tu wamekuteka katika ulimwengu wa roho.

Mathayo 16:19 "Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni."

4. Kufichwa katika magereza.

Kuna kifungo cha giza kinaitwa gereza.

Inawezekana wewe uko katika gereza la madeni, kukataliwa,kudhalauliwa bila sababu, kutengwa n.k

Inawezekana ndoa yako iko gerezani, inawezekana uchumba wako uko gerezani, iinawezekana biashara yako au wito wako viko gerezani.

Ndugu leo hakikisha unandoka katika gereza la kipepo ulimofungwa kipepo.

Omba au ombewa na watumishi waaminifu wa KRISTO na utatoka katika kifungo hicho.

Mathayo 7:7 "Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;"

5. Mawindo.

Kuna kifungo kinaitwa mawindo, inawezekana wewe siku zote uko katika mawindo ya majini au wachawi.

Kuna watu huwa hawalali usiku kwa sababu wako katika mawindo ya wachawi na majini.

Mathayo 18:18 "Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni."

Ndugu kumbuka kwamba YESU alikuwa anaziamuru nguvu za giza ziwatoke watu na zinatoka.

Luka 4:36 "Mshangao ukawashika wote, wakasemezana wakisema, Ni neno gani hili, maana awaamuru pepo wachafu kwa uwezo na nguvu, nao hutoka."

Mchungaji Laurent Mpoma


MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUJIFUNZA MANENO YA MUNGU.


TUNA MCHANGO WA UNUNUZI VIFAA KWA AJILI YA MKUTANO WA INJILI

1: SPIKA-------TSHS, 800,000/=

2: MAIKI 2 ZA WIRELESS....TSHS, 150,000/=

3: MAIKI 2 ZA WIRE......TSHS, 50,000/=

4: VITAMBAA VYA MADHABAHU.....TSHS, 60,000/=

KAMA UTAGUSWA KUCHANGIA KWA AJILI YA KUHUBIRI INJILI WASILIANA NA MCHUNGAJI KWA NAMBA:

AIRTEL: +255782859946.....JINA: LAURENT MPOMA

VODA: +255762756542........JINA: LAURENT MPOMA

TIGO: +255714890889..........JINA: LAURENT MPOMA

Mchungaji atakuombea na Mungu atakufungua....AMINA

===================================================================

MAOMBI NA MAOMBEZI

PIGA: +255762756542

WHATSAP: +255762756542

YOUTUBE: "upenyo Wa Mungu Tv". Kisha bonyeza "SUBSCRIBE"


Angalia Mkutano Mkubwa uliofanyika Singida Vijijini (MIPILO) MAGHOJOA, WATU WALIFUNGULIWA KWA JINA LA YESU WAKAWA HURU.

Post a Comment

0 Comments