Follow us

JINSI YA KUTOKA KWENYE VIFUNGO VYA GIZA.

Tangazo

 

JINSI YA KUTOKA KWENYE VIFUNGO VYA GIZA.

Kifungo cha kipepo

Kifungo cha kipepo ni adhabu ya mtu kuwekwa jela kipepo na mawakala wa shetani.

Wako watu wengi tu wanateswa na vifungo vya giza katika maisha yao, wengine wanatamani watoke katika vifungo hivyo lakini imeshindikana maana wanaenenda kimwili na sio kiroho.

Zaburi 142:7 "Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki watanizunguka, Kwa kuwa Wewe unanikirimu."

Jambo la kwanza kabisa nataka kukuambia ni kwamba Bwana YESU alikuja ili kuzivunja na kuziharibu kazi zote za shetani vikiwemo vifungo vya kipepo.

1 Yohana 3:8b "Kwa kusudi hili Mwana wa MUNGU alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi."

VIFUNGO HIVYO VYA GIZA.

1. Kuibiwa ufahamu kipepo ili ulitumikie kusudi la shetani na sio la MUNGU.

Kuna watu wengi fahamu zao zimefungwa kipepo kiasi kwamba wanalitumikia kusudi la shetani na sio la MUNGU, Leo kwa njia ya maombi yako katika jina la YESU KRISTO hakikisha unakiharibu kifungo hicho cha giza kilichokufunga ufahamu.

2 Wakorintho 10:4-5 " (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)

 tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya MUNGU; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii KRISTO;"

2. Kutekwa na nguvu za giza.

Baadhi ya dalili ya mtu aliye katika kifungu cha kutekwa na nguvu za giza ni kuonewa sana na majini au wachawi kwa sababu tu wamekuteka katika ulimwengu wa roho.

Mathayo 16:19 "Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni."

4. Kufichwa katika magereza.

Kuna kifungo cha giza kinaitwa gereza.

Inawezekana wewe uko katika gereza la madeni, kukataliwa,kudhalauliwa bila sababu, kutengwa n.k

Inawezekana ndoa yako iko gerezani, inawezekana uchumba wako uko gerezani, iinawezekana biashara yako au wito wako viko gerezani.

Ndugu leo hakikisha unandoka katika gereza la kipepo ulimofungwa kipepo.

Omba au ombewa na watumishi waaminifu wa KRISTO na utatoka katika kifungo hicho.

Mathayo 7:7 "Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;"

5. Mawindo.

Kuna kifungo kinaitwa mawindo, inawezekana wewe siku zote uko katika mawindo ya majini au wachawi.

Kuna watu huwa hawalali usiku kwa sababu wako katika mawindo ya wachawi na majini.

Mathayo 18:18 "Amin, nawaambieni, yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni."

Ndugu kumbuka kwamba YESU alikuwa anaziamuru nguvu za giza ziwatoke watu na zinatoka.

Luka 4:36 "Mshangao ukawashika wote, wakasemezana wakisema, Ni neno gani hili, maana awaamuru pepo wachafu kwa uwezo na nguvu, nao hutoka."

 

 

A.   Jinsi ya kutoka kwenye kifungo cha magonjwa.

Nilifunuliwa vitu hivi hapa chini hivyo wewe anayeumwa fanyia kazi utapona katika jina la YESU KRISTO.

1. Kwa maombi tubu kwa kilichosababisha ufungwe kifungo cha magonjwa.

Matendo  3:19 "Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake BWANA;"

2. Kwa maombi amuru ugonjwa utoke ndani yako.

Mfano hai Ni huu ambapo kiwete alipona.

Matendo  3:6-8 " Lakini Petro akasema, Mimi sina fedha, wala dhahabu, lakini nilicho nacho ndicho nikupacho. Kwa jina la YESU KRISTO wa Nazareti, simama uende. Akamshika mkono wa kuume, akamwinua, mara nyayo zake na vifundo vya miguu yake vikatiwa nguvu. Akaondoka upesi akasimama, akaanza kwenda; akaingia ndani ya hekalu pamoja nao, akienda, akiruka-ruka, na kumsifu MUNGU."

3. Omba MUNGU akuponye ugonjwa yaani akuondolee ugonjwa huo.

Kumbu 7:15 "Na BWANA atakuondolea ugonjwa wote; wala hatatia juu yako maradhi yo yote mabaya uyajuayo ya Misri, lakini atayaweka juu ya wote wakuchukiao."

4. Isemeshe nafsi yako kwamba unapona.

Mfano hai ni huyu aliyekuwa anaisemesha nafsi yake.

Zaburi 42:11 "Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini MUNGU; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na MUNGU wangu."

Hata wewe kwa jina lako iambie nafsi yako, itamkie nafsi yako uponyaji maana hayo Ni maombi na pia maneno yanaumba, mfano Mimi jina langu ni Peter Michael Mabula naweza kusema hivi "Peter usiogope maana muda mfupi ujao utapona, Peter usijali maana utanyunyuka tena, Peter Pokea uponyaji katika jina la YESU KRISTO n.k"

Hapo unakuwa unaisemesha nafsi yako na unakuwa unaiumbia uzima.

Ni muhimu Sana kuwa na maombi ya namna hii.

5. Kwa maombi ita afya itokayo kwa MUNGU.

Yeremia 33:6 "Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli."

B. Jinsi  ya kutoka katika vifungo vya dhambi.

1. Tubu na kuziacha dhambi zote.

Zaburi 34:14 "Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie."

 2. Vunja uhusiano  na watu  ulioshirikiana nao kwenye dhambi.

Zaburi 1:1 "Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha."

3. Amua kuwa mtu wa ibada na maombi.

Yohana 4:24 "MUNGU ni ROHO, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli."

4. Ishi maisha matakatifu ya wokovu wa KRISTO YESU.

1 Petro 1:15 "bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote;"

5. Usikumbuke mambo ya kwanza yaani mambo ya  dhambi.

Isaya 43:18 "Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani."

6. Enenda kwa ROHO MTAKATIFU.

Warumi 8:14 "Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU."

7. Haribu kwa damu ya YESU kila madhabahu ya giza au nguvu za giza zilizokuwa zinakutumikisha kufanya dhambi.

Kumbu 7:5 "Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomosheni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga."

C. Jinsi ya kutoka kwenye Vifungo vya madeni.

1. Omba MUNGU upate pesa ya kulipa kisha lipa deni hilo.

Mfano hai Ni mama huyu ambaye alitendewa muujiza na MUNGU kupitia Elisha kisha akalipa madeni.

2 Wafalme 4:7" Ndipo akaja akamwambia yule mtu wa MUNGU. Naye akasema, Enenda ukayauze mafuta haya, uilipe deni yako; nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako."

2. Epuka kukopa.

Mithali 22:7b "....  Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye."

3. Omba MUNGU akubariki na  fanya kazi kwa bidii ili uwe na pesa zako mwenyewe.

Mfano hai Ni huu.

Mwanzo 26:12-13 "Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, akapata mwaka ule vipimo mia kwa kimoja, BWANA akambariki. Na mtu huyu akawa mkuu, akazidi kusitawi, hata akawa mkuu sana."

4. Haribu kila nguvu za giza zinazoleta uharibifu maishani mwako ili ukope pesa kushughulikia matatizo yako.

Zaburi 142:7 "Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki watanizunguka, Kwa kuwa Wewe unanikirimu."

D. Jinsi ya kutoka katika Vifungo vya ajali au balaa au mikosi.

1. Haribu kwa maombi kila watenda kazi ya kishetani wanaotumika kuleta ajali, mikosi au balaa kwako.

Luka 10:19 "Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru."

2. Haribu madhabahu za giza zinazoleta  mambo yao kwako.

Kumbu 12:2-3 " Vunjeni kabisa mahali pote walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa mtakayoyamiliki, juu ya milima mirefu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti wenye majani mabichi; nanyi zivunjeni madhabahu zao, zibomoeni nguzo zao, na maashera yao yateketezeni kwa moto, na sanamu za kuchonga za miungu yao zikateni; na jina lao lifutilieni mbali na mahali hapo."

3. Mtegemee MUNGU na kumtumaini kisha omba  yeye akulinde.

Isaya 26:3-4 " Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini. Mtumainini BWANA siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele."

4. Kila siku omba katika jina la YESU na kabla ya jambo lolote au safari yeyote omba kwa MUNGU.

Mathayo 21:22 "Na yo yote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea."

5. Msikilize ROHO MTAKATIFU ili kama kuna mahali hatakupa amani kwenda basi usiende.

Zaburi 32:8 "Nitakufundisha na kukuonyesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama."

E. Jinsi ya Kutoka katika Kifungo cha kutokuzaa.

1. Omba Bwana YESU akufungue kifungo hicho.

Luka 4:18 "ROHO wa BWANA yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,"

2. Kwa maombi Haribu kila nguvu za giza zilizoitumika kukuzuilia uzao.

Yeremia 1:10 "angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ......."

Wakati mwingine tumia damu ya YESU KRISTO ili iende kwenye tatizo maana hujui ni wapi umefungwa ili iondoe tatizo.

3. Kwa maombi Futa kila maneno ya watu mabaya waliyokutamkia ili kukuzuia kuzaa.

Mithali 18:21 "Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; ......."

4. Kwa maombi Fungua tumbo lako la uzazi kwa maombi na takasa kila sehemu ya mwili wako na ya mume/mke wako inayohusika na uzao.

Mwanzo 25:21 "Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba."

5. Kwa maombi ita uzao wako kwa jina la YESU KRISTO.

Zaburi 113:9 "Huweka nyumbani mwanamke aliye tasa, Awe mama ya watoto mwenye furaha."

6. Kwa maombi ukomboe uzao wako uliozuiliwa kipepo ili usije.

Yohana 14:14 "Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya."

7. Mpinge shetani na kazi zake zote na uwe mtu wa maombi.

1 Petro 5:9 "Nanyi mpingeni huyo(shetani), mkiwa thabiti katika imani, ......."

8. Omba kwa MUNGU kwamba majira yako ya kupata uzao yaje na asizuie yeyote.

Mwanzo 17:21 "Bali agano langu nitalifanya imara kwa Isaka, ambaye Sara atakuzalia majira kama haya mwaka ujao."

9. Ishi maisha ya uaminifu katika ndoa yako huku ukifanyia kazi kimaombi  unavyoona kwenye ndoto au maono vinachohusika na uzao.

Waebrania 13:4 "Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi MUNGU atawahukumia adhabu."

10. Ita ahadi ya MUNGU ya uzao kwako ili itimie.

Mwanzo 1:28 "MUNGU akawabarikia, MUNGU akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi."

11. Omba kujua  mapenzi/Matakwa ya MUNGU juu ya uzao wako.

Mfano Ni hii familia ambayo ni MUNGU mwenyewe ndiye aliyewafunga wasizae kwa sababu ya makosa yao.

Mwanzo 20:18 "Maana BWANA alikuwa ameyafunga matumbo ya watu wa nyumbani mwa Abimeleki, wasizae, kwa ajili ya Sara mkewe Ibrahimu."

Sasa Kama mfano unatoka katika familia ya namna hiyo unatakiwa kutubu Sana na kuuliza mapenzi ya MUNGU juu ya wewe kuzaa.

12. Omba MUNGU akupe uwezo wa kuzaa na nguvu za MUNGU zikufunike.

Waebrania 11:11 "Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu."

Huwa na uwezo wa MUNGU wa kumwezesha mtu kubeba mimba, inawezekana mawakala wa shetani walishakuondolea uwezo huo hivyo omba MUNGU akupe uwezo huo wa kubeba mimba na kuzaa.

Sarah alipokea uwezo wa kubeba mimba , na kabla ya hapo hakuwa na huo uwezo wa ki MUNGU wa kuzaa, omba upewe uwezo wa kuzaa.

13.  Iondoe ndani yako roho ya kuharibu mimba na roho ya utasa.

Kutoka 23:26 "Hapatakuwa na mwenye kuharibu mimba, wala aliye tasa, katika nchi yako; na hesabu ya siku zako nitaitimiza."


                                                           MUNGU AKUBARIKI SANA 

MAOMBI NA MAOMBEZI

PIGA SIMU 
mchungaji laurent Mpoma
0763652896
watsap: 0763652896

Video ya Maombi na Maombezi kwenye mkutano mkubwa uliofanyika ilikuwa hivi ingia hapa>>>>https://youtu.be/fXkq6vZIa5A




Post a Comment

0 Comments