Follow us

FAIDA YA UNYENYEKEVU.

Tangazo

 

Mchungaji Laurent Mpoma

Somo: FAIDA YA UNYENYEKEVU.

1 Petro 5:5

Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.

Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;

Siraha kubwa ya kuinuliwa na kuheshimishwa ni unyenyekevu. Mtu mwenye kiburi ni adui wa Mungu. Mungu hashikamani na mtu au watu wenye kiburi.

Wafilipi 2:8-9

tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.

Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina;

Yesu hakuwa mwanadamu wa kawaida lakini alikuwa mnyenyekevu mbele ya wanadamu wa kawaida. Yesu aliweza kuwafanya vipofu waone, Yesu aliweza kuwafanya viziwi wasilikie, viwete watembee nk.

Maana yake Yesu angeweza kumfanya mtu anayeona awe kipofu, mtu anayesikia awe kiziwi, mtu anayetembea awe kiwete. Kwanini? Kwa sababu anawezaje kumfanya kiziwi asikie na ashindwe kumfanya anayesikia awe kiziwi? Alikuwa na uwezo wa kuwafanya adui zake wawe vipifu na wangekuwa vipofu, lakini alinyenyekea mbele ya wanadamu na kunifanya hana nguvu hana utukufu.

Kumbukumbu la Torati 8:12.

[12]Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake;

[13]na makundi yako ya ng’ombe na kondoo yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu ulicho nacho kitakapoongezeka;

[14]basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau BWANA, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa;

[15]aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika mwamba mgumu,

[16]aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako.

[17]Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo.

[18]Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

Watu wakishiba mioyo yao huinuka, kiburi huinuka. Mali zinapoongezeka ndipo na kiburi kinazaliwa ndani yao. Fedha inapoongezeka nipo na kiburi kinazaliwa ndani yao na kuanza kujitukuza na kujiinua kana kwamba ni kwa nguvu zao wameweza kumiliki mali nyingi.

Maandiko katika biblia yanasema. Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake; basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahaba BWANA, Mungu wako akupaye nguvu za kuoata utajiri.

Wengi wetu mioyo yao hubadirika ghafla kwa sababu ya fedha inapoongezeka, kwa sababu ya mshahara anaomiliki nk fedha inakua na nguvu moyoni mwake kuliko Yesu. Kabla hajawa na fedha, Yesu alikuwa na ngugu moyoni mwake kuliko fedha.

1 Petro 5:5 Mungu huwapinga wenye kiburi huwapa wanyenyekevu neema.

Mungu akubariki sana kwa kufuatilia Blog hii.

MCHUNGAJI WA FPCT MUNUNG'UNA AKIIMBISHA SIFA. KUONA BONYEZA KATIKA VIDEO HII HAPA CHINI.



Post a Comment

0 Comments