SOMO: NJIA TANO ZA KUMJUA MUNGU VIZURI.
Inawezekana
umeokoka na Yesu anaishi ndani...ila inawezekana pia haujamjua huyu Yesu
vizuri. kudhibitisha haya soma Marko 4:35-41, utaelewa. ukisoma mstari wa 41
unasema" wakaingiwa na hofu kuu, wakaambiana, ni nani huyu hata upepo na
bahari humtii?
Hapo tunaona
kwamba wanafunzi wa yesu walikua nae siku zote, waliona miujiza yake, ishara na
maajabu lakini siku ya dhoruba walishangaa kuona upepo na bahari
vikimtii.......!!!! kwaiyo hawakumjua Yesu vizur. nimepata mafunuo katika njia
za kumjua Mungu vizur.
1
KUMTAFUTA KWA BIDII
Mithali 8:17
inasema" nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii
wataniona. hapa anasema kuwa anatupenda...inawezekana unampenda Mungu na kwanza
sidhani kama kuna mtu ukimuuliza kama anampenda Mungu atakujibu kuwa Hampendi,
wote watasema wanampenda ila ukiendelea anasema wanaomtafuta kwa bidii ndio
watakao muona. nikagundua kuwa kuna tofauti ya KUMPENDA, KUMTAFUTA na KUMTAFUTA
KWA BIDII. inawezekana unampenda na unamtafuta, sasa nataka uweke bidii ili
uweze kumwona. Zaburi 105:4 inasema "mtakeni Bwana na nguvu zake,
utafuteni uso wake sikuzote......sasa hapa bidii iko wapi? ni pale alipomalizia
kwa kusema SIKUZOTE! Mithali 13:4 inasema "nafsi ya mtu mvivu hutamani asipate
kitu bali nafsi ya mwenye bidii itanenepeshwa.
2
KUMTAFUTA KWA MOYO WAKO WOTE
Kuna nyimbo
tulikua tunaimba inasema" jesus is number one, is everything to me! sijui
kama huwa unamaanisha ukiimba hii nyimbo? Yeremia 29:13 inasema" nanyi
mtanitafuta na kuniona, mkinitafuta kwa moyo wenu wote" hapa anamaanisha
kuwa u give up everything just to have him. kumbuka Mathayo 6:33, sasa watu
wanaigeuza hiyo na kuweka mambo yao mengine mbele.
Kumb 4:29
inasema"lakini huko, kama mkimtafuta BWANA Mungu wako utampata, ukimtafuta
kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote. Mathayo 22:37-38 inasema"
akawaambia mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote,
na kwa akili yako yote. ni ngumu wapendwa kumjua Mungu ipasavyo kama bado
hatufanyi kama maandiko yasemavyo....Bwana atusaidie!!!!
3 KULIJUA
NENO LAKE
mwalimu
anapofundisha wanafunzi darasani huwa anawaachia notes wakasome...unajua
kwanini? ili walijue lile somo vizuri kama isingekua ivyo basi ingeishia
darasani tu na mtiani unakuja. sasa hivyo hivyo, mafundisho kanisani hayatoshi
lazima tuwe na muda wa kumtafuta Mungu kupitia maandiko yaani NENO LAKE!
Mathayo 22:29 inasema" Yesu akajibu akawaambia, mwapotea kwa kuwa hamjui
maandiko wala uweza wa Mungu. inamaana kupotea kwetu inasababishwa na kutokujua
neno la Mungu na kwa kulijua neno la Mungu inatusaidia kumjua zaidi na zaidi.
Soma Mithali 2:1-5...mstari wa 5 unasema" ndipo utakapo fahamu kumcha
Bwana na kupata kumjua Mungu.
4 KUISHI
MAISHA MATAKATIFU
Mungu
anaheshimu sana watakatifu...sijui kama unajua hilo! soma Zaburi 25:14
inasema" siri ya Bwana iko kwa wale wamchao, na yeye atawajulisha agano
lake" sasa unataka nini tena? neno li wazi Mungu ukiwa karibu na Mungu kwa
maana ya utakatifu, utamjua Mungu vizuri. ipo mifano ya kina henoko, eliya n.k.
5 KUWA NA
ROHO MTAKATIFU
inawezekana
ukawa unaishi kumbe roho alishaondokaga zamani, pengine ulijichafua akakuacha
maana we ni hekalu lake! Wakorintho 2:10-11 inasema" lakini Mungu
ametufunulia sisi kwa Roho, maana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu.
maana ni nani katika binadamu ajuaye mambo ya binadamu ila roho iliyo ndani
yake? vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna afahamuye ila Roho wa Mungu.
MAOMBI NA MAOMBEZI
WASILIANA NA MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
+255763652896,
WATSAP: +255762756542
0 Comments