Follow us

NJIA ZA KUPIGANA VITA VYA KIROHO

Tangazo

Katika maombi ni muhimu sana kujua mambo yafuatayo.

1.      Kuomba kwa imani

 Waebrania 11:6 '' Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.'' Hautakiwi kuomba kwa imani tu bali omba kwa imani ukiwa msafi kwa MUNGU.  Mathayo 5:8 '' Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona MUNGU. '' Wenye moyo safi ni watakatifu waliosafishwa kwa damu ya YESU KRISTO, hao ndio wakiomba kwa imani wanaweza kumwona MUNGU vyema katika maisha yao.  Waebrania 12:14 '' ....... na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao; ''

Hivyo ni lazima uwe na Imani maana pasipo Imani haiwezekani kumwona Mungu.

Hivyo wewe Muombaji shika kanuni hiyo ya kiroho kwamba ''Pasipo imani siwezi kumpendeza MUNGU na pasipo utakatifu siwezi kumwona MUNGU''

Biblia inasema katika Yohana 1:18 '' Hakuna mtu aliyemwona MUNGU wakati wo wote; MUNGU Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba(MUNGU), huyu ndiye aliyemfunua.''  Kumbe Hakuna mwanadamu awezaye kumwona MUNGU kwa sura lakini Mathayo 5:8 inasema wenye moyo safi yaani watakatifu watamuona MUNGU, Yaani watakatifu wataingia uzima wa milele na kumwona MUNGU lakini pia watakatifu watasikiwa na MUNGU na kutendewa muujiza.

 2.      Kuomba katika jina la YESU KRISTO.

 Kuomba katika jina la YESU KRISTO inajumuisha mambo mawili. 

A. Kuomba ukilitaja na kulitegemea jina la YESU ili ushinde. Yohana 14:13 ''Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu(YESU KRISTO), hilo nitalifanya, ili Baba(MUNGU) atukuzwe ndani ya Mwana. ''

 Yohana 15:16 ''Si ninyi mlionichagua mimi(YESU), bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba(MUNGU)kwa jina langu awapeni. ''

 2 Timotheo 2:19 ''Lakini msingi wa MUNGU ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana(YESU) na auache uovu.''

3.      Kuomba katika ROHO MTAKATIFU. 

Kuomba katika ROHO MTAKATIFU inajumuisha mambo mawili. 

1. Kunena kwa lugha katika ROHO MTAKATIFU.  Marko 16:16-17 "Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; WATASEMA KWA LUGHA MPYA;"

 2. Kuomba kwa kuongozwa na ROHO MTAKATIFU au kujulishwa na ROHO MTAKATIFU.  Yuda 1:20 "Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo takatifu sana, na kuomba katika ROHO MTAKATIFU,"

 MUNGU AKUBARIKI SANA 

TUMA MAHITAJI YAKO 

WASILIANA NA MCHUNGAJI LAURENT MPOMA KWA MAOMBEZI.

0762756542

WATSAP: 0762756542


Post a Comment

0 Comments