NJIA MUHIMU KATIKA KUKUA KIROHO
1.KUWA
MHUDHURIAJI WA IBADA.
Isaya 9:6: Yesu ni
Mungupamoja na yeye kuwa Mungu katika mwonekano wa kuvaa mwili wa
kibinadamu, Yesu Kristo alikuwa akihudhuria kila palipokuwa ni mda wa kusali,
alikuwa akienda kusali kwenye masinagogi (makanisa ya Wayahudi )
Alitambua wazi kuwa Mkristo asipozingatia
ibada hawezi kukomaa na kuimarika kiroho pia watu wanapokusanyika kwa ajiri ya
Bwana Mungu naye huwepo katika hilo kusanyiko
( MATHAYO 18:20)
Tuangalie kitabu cha
KUMBUKUMBU
LA TORATI 12:5
mungu
anawaagiza wana wa islaeli kuwa mahali atakapo pachagua bwana Mungu aweke jina
lake maana ni makao yake "ELEKEZENI NYUSO ZENU PALE NA MWENDE HUKO"
neno hili
linatufundisha kwamba sehemu ambayo Mungu amechagua na akajenga madhabahu yake
(kanisa) kupitia makuhani Wake (wachungaji) ni lazima tukusanyike pale tumwabudu
na kumtukuza yeye maana pale ndio makao yake na anasema nasi kupitia madhabahu
yake hiyo (kanisa )tukusanyike pale tumwabudu. Bila ibada kiroho chako
kitadumaa kamwe huwezi endelea mbele.
WAEBRANIA 10:25
neno
linaendelea kutuhimiza tusiache kukusanyika kama ilivyo desturi yetu kua siku
za ibada ni lazima tukusanyike kanisani tumwabudu Mungu wetu.
2.KUPOKEA KIPAWA CHA ROHO MTAKATIFU
Yesu
aliwaagiza wanafunzi wake wasitoke yerusalem waingojee ahadi ya Baba ambayo ni
Roho Mtakatifu, akaendelea kusema mtapokea nguvu Roho Mtakatifu atakapo wajiria
juu yenu ndipo sasa mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, uyahudi, Samaria
na hata mwisho wa nchi.
Kumbe ili
tukue kiroho yatupasa tupokee kipawa cha Roho Mtakatifu.
WARUMI 8:9
anasisitiza kusema mtu yeyote asiye na huyo Roho wa Mungu mtu huyo hatambuliwi katika ufalme wa Mungu. (huyo si Wake kabisa)
3. KUJITOA
SADAKA WEWE PAMOJA NA MALI ZAKO .
WARUMI
12:1-2
paulo
anawaandikia kanisa la kumi kuwa "itoeni miili yenu kuwa dhabihu iliyo
hai, takatifu ya kumpendeza Mungu.
Neno la
Mungu linatufundisha kuitoa miili yetu kuwa dhabihu takatifu yaani mtu ajitoe
kwa ajiri ya Yesu, asiangarie mambo yake mwenyewe bali ajitoe, ajidhabihu mbele za Mungu ajihesabie si kitu
bila Yesu na ajitoe kwa kazi ya Mungu kwa moyo wote na kwa mali zake zote alizo
nazo
MATENDO
10:1-4
bibilia
inazungumza habari za mtu mmoja jina lake aliitwa Kornelio, Kornelio alikuwa
akimcha Mungu yeye na nyumba yake daima, Alikuwa akitoa sadaka nyingi na
kuwasaidia watu wenye uhitaji.
Ikumbukwe
kwamba wakati huo Kornelio alikuwa ni mtu wa mataifa ambao Mungu alikuwa bado
hajawapa neema ya kumjua yeye kwani wokovu kwa wakati huo alikuwa ni kwa
Wayahudi peke yao.
hivyo ili tufikie mafanikio makubwa sana ya kiroho ni lazima tujitoe na tuwe watoaji wa sadaka mbele za Mungu na ndipo tutakua, tutastawi sana ktk maisha yetu ya kiroho na kimwili.
Mungu akubariki na kukuzidishia katika kila
jambo ufanyalo wewe uliyetoa mda wako kusoma somo hili, MUNGU ASIKUPUNGUKIE BALI AKUKUMBUKE KATIKA
KAZI ZAKO ZOTE NA UFANIKIWE KATIKA JINA
LA YESU KRISTO
MUNGU
AKUBARIKI SANA KWA KUJIFUNZA MANENO YA MUNGU
Pakua APP yako sasa iliyijaa mafundisho ya Neno la MUNGU…. Hapa katika link
hii>>>>https://play.google.com/store/apps/details?id=com.mchungaji.laurent.mpoma”
YOUTUBE: KUANGALIA VIDEO ingia hapa >>>>”https://www.youtube.com/channel/UCjXjSSDOweHXL3YE5edBNIg”
MAOMBI NA MAOMBEZI
WASILIANA NA MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
+255763652896
Watsap: +762756542
0 Comments