KUTEMBEA KATIKA UWEPO WA MUNGU
Siri kubwa
ya mafanikio ya watakatifu wengi tunaowasoma kwenye biblia ilikuwa ni KUTEMBEA
KATIKA UWEPO WA MUNGU. Watumishi wengi wa Mungu tunaowaona wamefanikiwa kiroho
na ki-mwili siri yao kubwa ni kutembea katika uwepo wa Mungu.
Je, unataka
Mungu asaidie hatima yako? Je, unataka kupata ushindi dhidi ya matatizo makubwa
yanayokukabili?
Kama unataka
mafanikio;kama unataka upenyo kwenye maisha yako ni lazima utambue NGUVU YA UWEPO WA MUNGU na UTEMBEE KATIKA
UWEPO WAKE.
Hebu soma
kitabu cha Kutoka 33:13-15
Kutoka
33:13-15,"..Naye akamwambia, Uso wako USIPOKWENDA PAMOJA NAMI, USITUCHUKUE
KUTOKA HAPA."
Huyu alikuwa
ni Musa akimsihi Mungu aende naye kwenye safari ya kuwatoa wana wa Israeli
Misri na kuwapeleka kwenye nchi ya ahadi. Ukisoma kwa umakini kuanzia msitari
wa 13 hadi 15 unaweza kuelewa kwa undani na kupata siri kubwa.
Musa
hakuomba ishara na maajabu au miujiza wakati huu bali alimuomba MUNGU amwoneshe
njia na sio tu kumwonesha njia bali kutembea pamoja naye.
Na Mungu
alimjibu Musa kuwa UWEPO WAKE UTAENDA NAYE.
Wakristo
wengi wanapuuza sana kuhusu uwepo wa Mungu.Wengi hawaoni umuhimu wa Uwepo wa Mungu.Hata watumishi wengi wa
Mungu hawajui kuhusu NGUVU YA UWEPO WA MUNGU.
Kuwa na
UWEPO WA MUNGU ni jambo la msingi kuliko fedha na dhahabu.Kutembea na UWEPO WA
MUNGU kuna thamani kuliko UMAARUFU.
Uwepo wa
Mungu ukiwa juu yako unaweza kwenda popote. Uwepo wa Mungu ukiwa juu yako
hutahitaji kutafuta miujiza na ishara bali miujiza itakufuata wewe.
Ni hatari
kuishi nje ya uwepo wa Mungu.Nje ya uwepo wa Mungu kuna Maradhi, umaskini,
kuchukiwa, kukandamizwa, kudharauliwa, hofu, dhambi n.k
Swali la
kujiuliza:Je, unatembea katika uwepo wa Mungu?Je, uwepo wa Mungu umetoweka
kwenye maisha yako?
Ni vema
ufanye juu chini kuhakikisha unatembea
na UWEPO WA Mungu.
Hebu tusome
Zaburi 51:11
•Zaburi
51:11,"Usinitenge na uso wako, wala roho yako mtakatifu usiniondolee."
This is a
powerful prayer.Ni ombi lenye nguvu. Mwandishi wa Zaburi alikuwa anasema kama
kuna kitu Mungu alikuwa anataka kumnyang'anya, amnyang'anye kila kitu lakini sio UWEPO WA MUNGU. Alikuwa
anamsihi MUNGU ASIMNYAMAZIE.Hata kama kuna kosa alilifanya na alitakiwa kutiwa
chini ya nidhamu;Alikuwa tayari kupokea adhabu yo yote lakini si kunyamaziwa na
Mungu.
Tunahitaji
uwepo wa Mungu kwenye maisha yetu.Uwepo wa Mungu ni muhimu kwenye maisha yetu
ya kila siku.
Musa alikuwa
akipambana na wana wa Israeli. Mara nyingi walikuwa wakimwinukia na kutaka
kumshambulia.Kuna wakati walitaka kumponda mawe lakini alikumbuka ahadi ya
Mungu juu yake aliyosema naye kuwa,"UWEPO WANGU UTAKWENDA PAMOJA
NAMI."
Hiyo ahadi
iliendelea kumpa nguvu ya kusonga mbele na aliweza kuwaongoza wana wa Israeli
salama.
Unapokuwa na
uwepo wa Mungu;hata kama ukikutana na changamoto yoyote hauta ogopa.
Ukitembea na
uwepo wa Mungu Hutatetereka.
• Leo
Wakristo wengi wanajikuta
wanashambuliwa sana na maadui kwa sababu hawatembei katika uwepo wa
Mungu.
• Biashara nyingi zinashambuliwa kwa sababu
hazina uwepo wa Mungu.
•Ndoa nyingi na familia nyingi zimeshambuliwa
kwa sababu hazina uwepo wa Mungu.
•Leo maadui
wamepata nguvu za kutudhuru kwa sababu ya kushindwa kutembea katika uwepo wa
Mungu.
•Leo maadui
wamejipenyeza kwenye maisha yetu kwa
sababu ya kushindwa kutembea katika uwepo.
Ni muhimu
mpendwa unayesoma huu ujumbe utie bidii katika kuutafuta uso wa Mungu na uwepo
wake.(Zaburi 105:4 )
JINSI YA KUTEMBEA NA UWEPO WA MUNGU
1.Okoka
kweli kweli. Acha dhambi.Acha kuhalalisha dhambi.Uwepo wa Mungu haukai kwa
wenye dhambi. Dhambi inatutenga na uso wa Mungu.
2.Usicheze
na muda wako wa maombi na kutafakari. (Don't play with your prayer and quiet
time)
Siku ina
masaa 24.Tenga muda wa maombi,kusoma neno na kutafakari ukuu na uweza wa Mungu.
Danieli alifahamu siri hii.Yeye alikuwa
akiutafuta uso wa Mungu mara tatu kwa siku.
•Daniel 6:10
3.Jenga
tabia ya kukusanyika na wenzako katika
ibada.Maana wawili au watatu na zaidi wanapokusanyika na kumwita Mungu kwa
imani.Mungu hushuka.Kuna umuhimu wa
kukusanyika katika ibada.
•Waebrania
10:25
4.Uwe na
shauku ya kumjua Mungu na tamani kukaa na kutembea na uwepo wa Mungu.
•Zaburi 42:1
5.Jifunze
kuwa na ushirika na Roho Mtakatifu.Roho Mtakatifu ni nafsi ya tatu ya Mungu.Ni
Mtu na si KITU.Ni Mungu anayetenda kazi na wanadamu sasa.(Ukitaka kufahamu
zaidi kuhusu Roho Mtakatifu;pata nakala ya kitabu kilichoandikwa na Nabii B.G
Malisa)
6.Mwombe
Mungu akuoneshe njia ya kufuata. Usifanye kitu kama hujamshirikisha Mungu.
Usifanye maamuzi magumu yanayohusu hatima yako kama hujamshirikisha Mungu.
Usiruhusu kuingiza mtu kwenye maisha yako kama hujamshirikisha Mungu.

0 Comments