SOMO: MAOMBI YA KUFUNGULIWA KUTOKA LAANA.
3Yoh 1:2.
Unaweza ukawa umeokoka lakini ukawa umefungwa na laana, badala ya kutembea ktk baraka za Kimungu.
Mathayo 15:13
kuwa."Kila pando asilolipanda Baba yangu wa Mbinguni litang'olewa".Laana ni pando kutoka ktk ufalme wa shetani ambao wewe umehusika au athari za Baba /babu zako. Laana zinaweza kuwa kikwazo cha kutembea ktk baraka za Mungu. Laana zinaleta mipaka ktk maisha ya mtu na zinamfanya asiweze Kufanikiwa. Laana ni mkataba unaompa mtu nguvu ya kushindwa.
Yeremia 1:10."
Angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa,na kuharibu na kuangamiza'. Ili kujenga na kupanda:
Zipo atua7 za mtu kufunguliwa kutoka ktk laana.
1)Tambua maeneo ya laana ktk maisha yako. Maeneo ya laana unaweza kuyapata kutoka ktk vyanzo na dalili za laana.
2)Unaitaji toba na msamaha kwa vile vitu ambavyo vimeleta laana.
3)Kukataa au kukanusha kwa kinywa chako mikataba ya laana na vifungo
Isaya 28:18
4)Wasamehe watu wote Waliokukose
Mathayo 18:25-34
5)Omba maombi ya kufunguliwa kutoka ktk kila laana ktk maisha yako. Biblia yasema, "Kila atakayeliitia jina la Bwana atafunguliwa
Yoeli2:32
6)Pokea kufunguliwa kwa Imani
Marko11:24,
Mathayo 21:22
7)Unaitaji kutoa pepo wachafu walioko nyuma ya laana
Marko 16:17-18.
ukihitaji maombi ya kufunguliwa tafuta watumishi wanaotumiwa na Mungu ktk huduma ya kufunguliwa.
0 Comments