Fahamu kuwa ni mpango wa Mungu kwa kila mtoto wake kufanikiwa na kustawi katika kila eneo la maisha yake; afya, biashara, kazi na taaluma, ndoa na familia na kila eneo (3 Yohana 1:2).
1. UNGAMANIKA NA MUNGU
Utajiri na mafanikio katika ufalme ni matokeo ya kuungamanika na Mungu (Ayubu 22-21-24). Chochote wengine wanachoteseka na kutoa jasho kutafuta unapoungamanika na Mungu kina kuwa ni fungu lako (Mathayo 6:25-33).
2. Elewa sheria/kanuni za fedha
Tafuta kujua namna ya kutengeneza pesa kwa kutumia sheria za Kiungu (Yohana 6).
3. Fanya kazi
Mafanikio na utajiri katika ufalme haupatikani kwa wasiofanya kazi au wazembe. Fanya kazi kwa bidii kwa kutendea kazi kanuni za Kiungu (Zaburi 1:1-3, Yoshua 1:8). Kumbuka kuwa mafanikio hupatikana mahala popote ikiwa utafanya kazi na Mungu
4. Wekeza
Kutegemea mshahara wa kazi yako uliyoajiriwa kamwe hakutakufanya ufanikiwe na kutajirika kama hutawekeza. Kazi hukupa mtaji ili uweze kuwekeza, usile mtaji wote, anza leo wekeza. Kile ulichanacho kinatosha kuanza kuwekeza ikiwa utafikiria vizuri. Mafanikio ya kifedha ni fungu la wale wanaowekeza katika biashara sio wanaotegemea mshahara (Mathayo 25:14-18).
5. Panda mbegu
Hakuna anayeweza kutarajia kuvuna pasipo na kupanda, kadri mkulima anavyozidi kuendelea kupanda kila msimu ndivyo anavyoendelea kuvuna (Mwanzo 8:22). Jiungamanishe na baraka za mafanikio ya kifedha katika ufalme kupitia njia ya kumtolea Mungu (2 Wakorintho 9:6).
6. Jenga utamaduni wa kuweka akiba
Mungu anaamini katika kuweka akiba (Mwanzo 41:36). Mtu asiyejiwekea akiba leo, kesho yake itakuwa mashakani (1 Timotheo 6:17-19)
7. Acha ufujaji wa mali
Hatima nzuri ya kifedha kesho ni kwa wale wanaoepuka ufujaji leo. Huwezi kutumia leo kupita kiasi na kesho ukawa na kitu cha kuonesha! Haiwezani. Ukitaka kufanikiwa katika ufalme, zingatia kuepuka ufujaji, usitumie mali kwa matumizi ambayo sio muhimu wala rasmi (Yohana 6:12)
MAOMBI NA MAOMBEZI
MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
PIGA: 0762756542
WATSAP: 0762756542
YOUTUBE:"https://www.youtube.com/channel/UCjXjSSDOweHXL3YE5edBNIg"
>>USISAHAU "KUSUBSRIBE" Ili kupata Video zote za mahubiri na mafundisho.

0 Comments