Follow us

SOMO : UAMSHO

Tangazo

                      

MCHUNGAJI LAURENT


SOMO : UAMSHO

Uamsho ni kanuni muhimu sana kwa ukuwaji wa kanisa na wokovu wa mtu binafsi.

MAANA YA UAMSHO (Revival)

Ni udhihirisho wa nguvu za Roho mtakatifu ambazo huleta UREJESHO KAMILI wa uzima wa kiroho na kimwili ktk maisha ya mtu.

Ni swala Zima la kuamshwa kiroho.

Mtu mwenye Uamsho lazima aongezeke ktk maeneo yafuatayo

1. Aongezeke kiroho (spiritual growth)

2. Aongezeke kiuchumi (financial growth)

3. Aongezeke kijografia (geographic growth)  kwa maana ya kanisa lazima lijiongeze kwa kuwa na matawi ktk maeneo mengine. Kama ni biashara lazima iongezeke toka ofisi moja na kuwa na matawi mengine ya ofisi maeneo mbali mbali.

Kanisa au mtu binafsi asiye na Uamsho hawaezi kufanya mambo yafuatayo.

i. Hawezi kufanya huduma ipasavyo

ii. Hawezi kuwa na nidhamu

iii. Hawezi kumwabudu Mungu kkt roho na kweli.

iv. Hawezi kujitawala, kujitegemea, na kujieneza.

DALILI ZA KUTOWEKA KWA UAMSHO.

(a) Kupoteza kiu ya maombi

(b) Kupoteza hamu ya ibada

(c) Kufanya kazi ya Mungu kwa ulegevu

(d) Kuingiwa na roho za uasi juu ya kweli na watumishi

(e) Kuanza kukubaliana (compromise) na mambo mayonge au dhambi ambazo hapo zamani ulizikataa

UAMSHO UNAWEZA KUTOKEA KTK MAKUNDI YAFUATAYO

i. Unaweza kutokea kwa mtu binafsi

ii. Unaweza kutokea ktkt ya kikundi au idara ndani ya kanisa.

iii. Unaweza kutokea juu ya kanisa zima la Mahalia pamoja.

iv. Unaweza kutokea juu ya kanisa la nchi nzima au hata ulimwengu mzima.

MAMBO MANNE YANAYORUDISHA UAMSHO

1.Tambua makosa yako kisha fanya toba ya kweli mbele za Mungu.

2.Uwe na shauku, kiu na njaa ya UREJESHO wa ulivyopoteza.

3.Utii juu ya Bwana na Neno lake

4.Uwe na Imani kwa Mungu

5. Omba bila kukoma juu ya Uamsho.

Kwa kufanya hivyo udhihirisho wa nguvu za Roho mtakatifu ambazo huleta UREJESHO KAMILI wa uzima wa kiroho na kimwili, yaani yale ulivyopoteza, utakuja juu yako nawe utajisikia furaha mpya juu ya maisha yako.

Ni maombi yangu kwamba vile viti vya thamani ulivyopoteza au kuviangusha ktk maisha yako ya wokovu, huduma yako, ndoa yako, biashara yako, masomo yako, maono yako. Na ktk maeneo mbali mbali ambayo sijayataja hapa BWANA Mungu aingilie kati na kufanya UREJESHO KAMILI ktk Jina la YESU KRISTO. I Wafalme 6:5-7. Lakini mojawapo alipokuwa ktk kukata boriti, chuma cha shoka kikaanguka majini(mtoni) akalia akasema Ole wangu Bwana wangu maana kiliazimwa kile. Mtu wa Mungu akasema kilianguka wapi? Akamwonyesha mahali. Akakata kijiti akakitupa palepale chuma kikaelea. Akasema kiokote. Basi akanyosha mkono akakitwaa.

 

MUNGU AKUBARIKI SANA

 

MCHUNGAJI LAURENT E. MPOMA

SOMA: 2 MAMBO YA NYAKATI 1:1-13. Utagundua iko faida kubwa sana unayoipata unapomtumikia Mungu kwa njia ya matoleo. Naomba nikushirikishe hizi Baraka maana Mungu anakubariki sasa, Anakwenda kufungua Milango yako ya Uchumi, Elimu, Nyota, Mashamba, Ndoa, Watoto wako na mengineyo mengi...Utabadilishwa kama sulemani alivyo ongea na Mungu Live usiku . na Wewe uko tayari kuwa kama Sulemeni?..Mguse Mungu ili na yeye akuguse.

TUNAUNUNUZI WA VIFAA HIZI KWA AJILI YA MKUTANO WA INJILI.

1. SPEAKER.......1....TSHS, 350,000/=

2. VITAA VYA MADHABAHU..........TSHS, 40,000/=

3. MAIKI .......WIRELESS......2.....TSHS, 100,000/=

4. VITI........10......TSHS, 160,000/=


UKIGUSWA KUMTOLEA MUNGU.

WASILIANA NA MCHUNGAJI

TUMIA:

0762756542....M-PESA.......JINA: LAURENT MPOMA

0714890889.....TIGO PESA....JINA: LAURENT MPOMA

0782859946.....AIRTEL MONEY......JINA: LAURENT MPOMA


KUTAKUWA NA MAOMBI KWA KILA MTU ATAKAYE MTOLEA MUNGU.


MUNGU AKUBARIKI SANA


MAOMBI NA MAOMBEZI

PIGA : 0762756542, 0782859942, 0714890889

WATSAP: 0762756542

                  0714890889


 


Post a Comment

0 Comments