MAOMBI YA MGUSO WA MUNGU SEHEMU YA PILI.
MUNGU AKUPIGANIE KTK UONEVU WOWOTE ULIO MBELE YAKO
Hapo ndipo Musa akawaita wazee wa Israeli, na kuwaambia, Nendeni, mkajitwalie wana-kondoo kama jamaa zenu zilivyo mkamchinje pasaka. Nanyi twaeni tawi la hisopu, mkalichovye katika ile damu iliyo bakulini na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni mwa nyumba yake hata asubuhi.
KWA KUWA BWANA ATAPITA ILI AWAPIGE HAO WAMISRI; NA HAPO ATAKAPOIONA HIYO DAMU KATIKA KIZINGITI CHA JUU, NA KATIKA ILE MIIMO MIWILI, BWANA ATAPITA JUU YA MLANGO, WALA HATAMWACHA MWENYE KUHARIBU AINGIE NYUMBANI MWENU KUWAPIGA NINYI. Nanyi mtalitunza jambo hili kuwa ni amri kwako na kwa wanao milele. Itakuwa hapo mtakapoifikilia hiyo nchi, Bwana atakayowapa, kama alivyoahidi, ndipo mtakapoushika utumishi huu. Kisha itakuwa, hapo watoto wenu watakapowauliza, N'nini maana yake utumishi huu kwenu? NDIPO MTAWAAMBIA, NI DHABIHU YA PASAKA YA BWANA, kwa kuwa alipita juu ya nyumba za wana wa Israeli huko Misri, hapo alipowapiga Wamisri, akaziokoa nyumba zetu. Hao watu wakainama vichwa na kusujudia. Basi wana wa Israeli wakaenda na kufanya mambo hayo; vile vile kama Bwana alivyowaamuru Musa na Haruni, ndivyo walivyofanya. SOMA: KUTOKA 12:21-28
Nakusalimu katika jina la Yesu Kristo.
Nisikilize mwana wa Mungu: Maombi haya ni maombi ya vita. Tunahitaji kupambana kuvuka hatua.
Sasa nina uzoefu watu wengi maombi ya kupambana hawajawa na uzoefu nayo. Nakuhitaji vifungu tunavyovitoa hakikisha unavitumia. Omba kwa kinywa chako. Kiri kwa kinywa chako.
Imeandikwa ‘Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka’ SOMA: MATHAYO 11:12. Sasa lazima kukubali kupambana hadi adui aachie kile alichokuwa amekishikilia katika ulimwengu wa roho kwako.
‘Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama’ SOMA: WAEFESO 6:12-13
Jana tulijikita kipekee kabisa kwenye maombi juu ya uchumi. Kuna shuhuda za watu wengi tulioomba nao tumemuona Mungu akidhihirisha mambo ya ajabu sana. Ndugu wakati sisi tunajisahau kumtumikia Mungu Shetani yuko kazini kwa kazi kubwa.
Mwana wa Mungu kama Bwana alivyopita juu ya nyumba za wana wa Israeli kuwapiga wamisri, Mruhusu na mwambie Mungu Malaika wake apite kama kumekuwa na uonevu kwenye eneo lolote ktk nyumba yako usiku au mchana mwambie Mungu malaika mwenye upanga apite katika nyumba yako apigane na adui hao. Mwambie malaika apite kwenye sehemu yako ya kazi, kwenye ndoa yako, kwenye chochote unachotaka Mungu apite akupiganie.
#ISAYA 37:36 “Basi malaika wa Bwana alitoka, akaua watu mia na themanini na tano elfu katika kituo cha Waashuri, na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe, hao walikuwa maiti wote pia”. Sikiliza ndugu, mwambie Mungu malaika apite na kuangamiza kila adui aliyeweka matuo kwenye kazi yako, kwenye biashara yako au kwenye nyumba yako.
Mwambie Mungu kama malaika alivyoshuka kwenye kituo cha waashuri na kuangamiza watu 185,000 mwambie angaamize kila majeshi ya maadui waliojificha eneo lolote kwenye maisha yako.
Mwambie usiogope.
Imeandikwa ‘Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele” SOMA: YOHANA 10:10. Mwambie Mungu eneo ambalo adui alikuwa amekubana, adui alikuwa amekuua, adui alikuwa amekuteka, adui alikuwa ameharibu, Mwambie Mungu malaika wako na apite katikati yangu sasa katika jina la Yesu. Mwambie kama Neno lako lisemavyo kuwa Yesu umekuja ili tuwe na uzima wa milele tena tuwe nao tele.
Ubarikiwe sana na Share ujumbe huu kama umebarikiwa na mwingine abarikiwe.
“Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao” SOMA: ISAYA 61:1-2
Kwa maombi na maombezi, unataka kupokea uponyaji au kufunguliwa kwenye kifungo chochote kile, ushauri au unatamani ujitoe kikamilifu kumtumikia Mungu na UNATAKA KUMPOKEA BWANA YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YAKO NA AKUSAMEHE DHAMBI ABADILISHE MAISHA YAKO NA TABIA MBAYA ZILIZOKUSHINDA
MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUJIFUNZA ZAIDI NA KUENDELEA KUFUATILIA MASOMO HAYA.
>>Maombi na maombezi piga: 0762756542, 0782859946, 0714890889
>>Maombi na maombezi piga: 0762756542, 0782859946, 0714890889
>>Tuma hitaji lako kwa namba hapo juu AU Watsap: 0762756542
>>E-mail: mchungajilaurent@gmail.com
>>Kupata video za mafundisho na mahubiri youtube ingia hapa>>"https://bit.ly/2wNLG8j" kisha usisahau "SUBSCRIBE" Kisha bofya kengele, ili uwe wa kwanza kupata video zetu zote.


0 Comments