Follow us

MAOMBI YA KUTENGUA VIAPO

Tangazo

MAOMBI YA KUTENGUA VIAPO

Kiapo kinaweza kumfunga mtu kwa lile jambo aliloliapia. Watu wengi maisha yao yameharibika kwasababu ya kutokutimiza viapo vyao walivyoapa.

wachawi ni binadamu kama wewe lakini nao huapa. Huloga watu hatakama hawapendi kwasababu ya viapo vya uchawi walivyoapa leo tunajifunza maana ya kiapo na nguvu zake baadae tunakwenda kuomba kwa jina la Yesu.

Kiapo ni maneno yaliyotamkwa yanayoweza kuleta laana juu ya mtu au familia.

Yoshua 6:26-27 “Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe mbele za Bwana mtu yule atakayeinuka na kuujenga tena mji huu wa Yeriko; ataweka msingi wake kwa kufiliwa na mzaliwa wa kwanza wake, tena atayasimamisha malango yake kwa kufiliwa na mtoto wake mwanamume aliye mdogo.Basi Bwana alikuwa pamoja na Yoshua; sifa zake zikaenea katika nchi ile yote.”

Aliwaapisha kwasababu hakuweza kuwaacha hivihivi ili mtu asije kujenga tena Yeriko na akijenga atafiwa. Kiapo kinaendana na taratibu zake na huyu anayekuapisha anasema ukifanya hivi na hivi yatakupata haya.

Siku hizi utakuta familia kila mwaka anakufa mtu maana yake kuna viapo vya kifamilia. Ukirudi nyuma miaka ya nyuma tulikua hatumjui Mungu hivyo wazazi wetu walikua wanafanya viapo kwa miungu na mashetani, viapo vile vimefata familia zetu mpaja leo hii.

1 Wafalme 16:30-34 “Ahabu mwana wa Omri akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana kuliko wote waliomtangulia.Ikawa, kama ingalikuwa neno dogo tu kuyaendea makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, akaenda akamtumikia Baali, akamsujudia.Akamjengea Baali madhabahu katika nyumba ya Baali, aliyoijenga huko Samaria.Ahabu akaifanya Ashera; Ahabu akazidi kumghadhibisha Bwana, Mungu wa Israeli, kuliko wafalme wote wa Israeli waliomtangulia.Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni.”

Kiapo ni maneno mamlaka ya mwisho ya kutoa. Unapomuona mtu amefikia kwenye kiapo maana yake ni mamlaka yake ya mwisho inambidi aape kwanza ndio aanze jambo fulani, hapa watu wengi wameshikiliwa.

Unakuta mtu analambabudongo anaapa au anaapa “haki ya Mungu kabisa nakuapia” na baadae hatimizi lile alilosema ndipo matatizo yanaanza kumpata. Mtu anatoa kiapo ili aeleweke, akubalike au afahamike kwa wakati ule.

Kama ulimwengu huu wa mwili unavyoongozwa na sheria ndivyo na kwenye ulimwengu wa roho unaongozwa na sheria. Sheria hizi sio kwamba zinamgandamiza mtu hapana bali zimewekwa ili kumlinda.

Mfano sheria za barabarani zimewekwa ili uwe mwangalifu usipatwe na ajali, wewe ukisema “mimi ni mtaalam na uzoefu Roho wa Bwana atanilinda ntalala na mia, ninaharaka, nataka niwahi” utajikuta umewahi mbinguni kama umeokoka au jehanam kama hujaokoka.

Biblia inasema mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi mkikataa mtaangamizwa kwa upanga. Unapojiingiza kwenye kiapo uwe inajua au hujui mashetani yanakukamata yanaangalia jambo gani likupate sababu umeapa au kuna mtu ameapa mambo fulani yakupate.

Mungu akitaka kufanya jambo na mtu anaapa kwamba anachokisema lazima kitatimia.

Isaya 45:22-23 Niangalieni mimi, mkaokolewe, enyi ncha zote za dunia; maana mimi ni Mungu; hapana mwingine.Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa.

Hakuna wokovu kwa mwingine awaye yeyote isipokua wokovu unaotoka kwa Mungu Yehova. Mungu anaapa kwa nafsi yake kila alilosema litatimia vilevile. Maana nyingine ya kiapo ni kujifunga nafsi yako.

Waebrania 6:13-16 “Kwa maana Mungu, alipompa Ibrahimu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake,akisema, Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza nitakuongeza.Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi.Maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao; na kwao ukomo wa mashindano yote ya maneno ni kiapo, kwa kuyathibitisha.”

Uharibifu huletwa ndani ya kiapo ikiwa aliyeapa kutenda jambo fulani hajalitimiza. Leo hii kuna viapo vinawasumbua watu na wengibe hawajui wanateseka kwasababu ya viapo flani walivyofanya.

KIRI KWA KINYWA CHAKO HAPO ULIPO.
"Kila kiapo kilichofanywa juu yangu ili kuniletea uharibifu nakisambaratisha kwa jina la Yesu Amen"



Anaapa kwa kusema maneno au kwa kutenda matendo na kuacha mahusihano akifikiri yupo salama lakini hayupo salama. Kwahiyo mapepo yanakua na taarifa zako za viapo ulivyoingia wanavitumia kukukwamisha usiende mbele wewe unashangaa kuna nini kumbe kuna viapo ulivyoingia ndivyo vinakukamata.

Unaweza kufanya mambo ukaondoka huku nyuma ukaacha alama na fahamu kila mtu anaadui zake na baadae adui zako wanakuja kupita nyuma waangalie ulipoacha alama zako ili wazitumie kukudhuru.

Ndiomaana ya kumuomba Mungu kutengua viapo vilivyo juu yetu kwa jina la Yesu. Danieli alipopandishwa cheo walitafuta sababu ya kuitumia ili wampige aanguke chini. Ashukuriwe Mungu kwa Danieli hawakupata sababu ya kumwangusha na kwasababu hiyo na wewe itokee hivyohivyo wasipate jambo la kukuangusha kwa jina la Yesu Amen.

Kulikua na binti aliyecheza vizuri mbele za Mfalme Herode mpaka Herode akaapa binti huyo aombe chochote atampa, binti yule mama yake alikua na ugomvi binafsi na Yohana na binti huyu akaenda kumwambia mama yake Herode ameambiwa na Mfalme aombe chochote atapewa. Mama yake akamwambia aombe kichwa cha Yohana.

Jambo hili likafanyika sababu Herode alikua amekwisha apa japo sio kwasababu alitaka au alipenda hapa kwasababu kuna nguvu ya kiapo ilimfanya afanye hivyo, kuna watu leo hii wanafanya uzinzi, wanaiba, wanasema uongo sio kwasababu wanapenda ni kwasababu kuna nguvu ya kiapo inawashikilia.

Nguvu ya kiapo ni pale watu wawili wanapokubaliana jambo wanafanya kiapo na mbinguni wanarekodi jambo hilo iwe ni mzaha au utani.

Mathayo 18:8  Basi mkono wako au mguu wako ukikukosesha, ukate ukautupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima hali umepungukiwa na mkono au mguu, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele.

Huku duniani hata kama ikitokea mmoja ametangulia mbele za haki rohoni bado hamtakua mmeachana sababu ya nguvu ya kiapo ambayo inaweza kuwafanya walio mbali warudi kukutana pamoja.

Mungu anapoapa juu ya jambo haijalishi umepigwa ukatupwa mbali wametawanya mwilini tu lakini rohoni uko palepale sababu kuna nguvu ya kiapo ya kukurudisha. Wana wa Israeli walitawanyika dunia nzima lakini sababu Mungu aliwaapia walirudi wakawa taifa moja.

Mungu aliwazuia watu wasiape sababu mtu akiapa lazima jamvo litokee. Kwebye ulimwengu wa roho chochote unachokisema lazima kitokee iwe ni bahati mbaya au hasira au masihara. Utatendewa vile ulivyosema.

Yakobo 5:12  Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; bali ndiyo yenu na iwe ndiyo, na siyo yenu iwe siyo, msije mkaangukia hukumu.

Kwasababu tunaishi kwenye ulimwengu mwili tunaishi na watu wenye akili lakini za kuzimu walipokwenda kuapa ili waipate, panapofikita mahala unatakiwa upate msaada huwezi kupata sababu kuna kiapo, mahali unapotakiwa upite huwezi kupita sababu kuna nguvu ya kiapo inayokuzuia usipite mpaka uingoe kwa damu ya Mwanakondoo.

Mfalme Dario alishindwa kumsaidia Danieli asitupwe kwenye shimo sababu alikua amekwisha apa na nguvu ya kiapo ndiyo ilikua imemzuia asimsaidie.

Nguvu ya kiapo inaweza kuzuia usipande ngazi na ili upande ngazi lazima awepo wa kukupandisha ngazi, shida anayoipata mtu wako huwa anatokewa na mapepo asikusaidie upande ngazi au kupata msaada fulani kwenye maisha yako. Mashetani na mizimu ya familia inamua kumwingia yule anayetakiwa kukusaidia usipate msaada. Ashukuriwe Mungu Danieli alikua vizuri na Mungu. Je mimi na wewe je Mungu akitaka kukusaidia anaangalia maisha yako jinsi yalivyo ya kuunga unga Mungu hawezi kukusaidia kama hauko vizuri na yeye, acha dhambi ili Mungu akusaidie kwa jina la Yesu.

Kama maisha yako hayako sawa na Mungu. Kama maisha yako hujasoma huna wa kukusaidia ni Mungu pekee ndiye atakayekusaidia. Maisha ya sasahivi kuna watu kama huna cha kumpa hawezi kukupa huu ni ulimwengu wa nipe nikupe, la sivyo uwatiishe waliokaa pale watishike wakupe kile unachokitaka kwa nguvu ya Mungu, unamwomba Mungu naye anakusikia na anakujibu kama alivyomjibu Danieli.

Daudi alikua na Mungu na Mungu alimsaidia. Ni bora uwe na Mungu ndani yako kuliko kuwa na namba za watu hamsini ambao ukiwa na tatizo hawawezi kukusaidia wanakuambia pambana na hali yako.
Maamiri na mawaziri waliapa kwamba Danieli hatatoka kwenye mtego wao lakini Mungu alimsaidia Danieli sababu Danieli alijua kuna viapo vyao juu yake, alikua anaomba siku tatu asubuhi, mchana na jioni aliomba na kuvunja viapo vyao na hata alilotupwa kwenye shimo la simba, simba hawakumdhuru sababu alikua amekwisha vunja nguvu ya kiapo.

Matendo ya Mitume 23:12  (Kulipopambauka, Wayahudi wakafanya mapatano, wakajifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala hawatakunywa hata wamwue Paulo).

Ukiwa na Mungu hata ukiwa ndani ya shimo wamo walewale waliokukataa watakukubali na walewale waliokutupa ndani ya shimo watakutoa. Ni kweli umekaa kama zoba huna mbele wala nyuma lakini saa yako inakuja utasimana tena kwa jina la Yesu utainuka tena utashinda, leo hii umekaa unaonekana umeoza huna kitu na hujasoma kila mtu anakaa mbali nawe usilie wala usilalamike.

UKIRI WA MAOMBI:-
“Kwa jina la Yesu nasimama kinyume na kila kiapo kilichoapwa juu yangu na familia yangu kwa damu ya Yesu, leo navunja maneno ya viapo walivyoniapisha kwenye maisha yangu kwa damu ya Yesu, viapo vya uchawi, viapo vya kishirikina, viapo nilivyoingia mimi mwenyewe bila kujua leo navivunja kwa damu ya mwanakondoo, navunja viapo vyote nilivyoingia na Watu kwa jina la Yesu navunja vipo vyao kwa damu ya Yesu imeandikwa nimepewa mamlaka ya kungoa na kubomoa kwa damu ya Mwanakondoo ninangvo viapo vilivyonishikilia kwa jina la Yesu, mwombe Mungu akusaidie omba kutengua viapo vyao tengua kiapo ulichoingia kwa jina la Yesu, tengua viapo kama Danieli alivyotengua viapo vyao na wewe omba kwa jina la Yesu tengua viapo vya umaskini, viapo vya magonjwa kwa jina la Yesu.”



ILI UWEZE KUOMBEWA NA KUFUNGULIWA  WASILIANA NA MTUMISHI WA MUNGU .

MAOMBI NA MAOMBEZI, Wasiliana na Mchungaji Laurent
Mchungaji Laurent
Simu :0762756542, 0782859942, 0714890889
Watsap: 0762756542
e-mail: mchungajilaurent@gmail.com

AU
YOUTUBE:"upenyo wa Mungu Tv" kisha Subscribe, gonga kengele.



MUNGU WA MBINGUNI AKUFUNGUE KATIKA VIAPO .

UBARIKIWE SANA NA MUNGU ALIYE HAI.



Post a Comment

0 Comments