Follow us

MAOMBI YA KUNG'OA MIPAKA YA ADUI ZAKO

Tangazo
MAOMBI YA KUNG'OA MIPAKA YA ADUI ZAKO

KISHA WEWE KUMWEKEA ADUI MIPAKA.

BWANA YESU atukuzwe.
Karibu tujifunze kisha tuombe maombi ya vita.

Leo nataka tuombe tuking'oa mipaka yote ambayo adui zetu wametuwekea, Kisha tuweke mipaka sisi ili adui asivamie kwetu.

Iko mipaka ya MUNGU ambayo ni mipaka mizuri na ya ushindi kwetu lakini mawakala wa shetani nao huweka mipaka yao ili kutuzuia.

Ayubu 38:11 '' Nikasema, Utafika mpaka hapa, lakini hutapita, Na hapa mawimbi yako
yanyetayo yatazuiliwa?'' Siku moja katika siku za karibuni ilikuwa ni zamu yangu kuomba ili kumaliza ibada ya mkesha.
Mipaka ni kizuizi katika jambo lako lolote. Ngoja nikupe maandiko machache ili yakusaidie kujua na kuomba
.
1 Thesalonike 2:18 ''wa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na Shetani akatuzuia.''

Katika andiko hilo Biblia inaonyesha wazi kwamba shetani wakati mwingine anaweza
kuwazuia wateule wa MUNGU katika mipango yao, Mtume Paulo alipanga kwenda kuhubiri katika mji fulani lakini mara mbili zote shetani alimzuia, maana yake shetani alimwekea mpaka mtumishi wa MUNGU ili asifanikiwe kuvuka kwenda kwenye kazi yake ya injili. Kizuizi kama hicho kinaweza kuwa katika maisha ya kila mtu, mipango yako ya mwaka huu inaweza kuzuiliwa na kama hutajua jinsi ya kung'oa mipaka hiyo ya
adui hakika mwaka utaisha wewe ukiwa hivyo hivyo.


Isaya42:22 '' Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika
mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye;
wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.''


Kuna siri nzito sana katika andiko hilo la Isaya
42:22.
Kuna watu wameibiwa ufahamu , kuna watu wametekwa na mawakala wa shetani.
Kuna watu wamenaswa katika mitego ya shetani. Kuna watu ndoa zao, kazi zao, masomo yao, familia zao au uchumba wao umenaswa katika mitego ya shetani. Kuna watu wako katika mashimo maana yake wako katika kifungo cha shetani. Kuna watu wamefichwa katika magereza ya magonjwa. Kuna ndoa ziko gereza la mateso. Kuna biashara za watu ziko katika gereza la kufilisika.


Ayubu 33:11 ''Hunitia miguu yangu katika mkatale, Na mapito yangu yote huyapeleleza.'' Hata maadui zako wanaweza kukupeleleza na
kukuwekea mipaka. Mkatale ni mti uliotumika kuwafunga watu ili wasitoroke.
Kuna watu shetani amewawekea mipaka ili wasifanikiwe kufikia malengo yao.

Leo tunang'oa mipaka yote ya kipepo kwa jina la

YESU KRISTO.
.

Ayubu 14:4-5 '' Ni nani awezaye kutoa kitu kilicho safi kitoke katika kitu kichafu? Hapana awezaye. Kwa kuwa siku zake zimeamriwa, hesabu ya miezi yake unayo wewe, Nawe umemwekea mipaka yake asiyoweza kuipita;'' Mipaka ipo.

MUNGU anaweza kukuwekea mipaka mizuri lakini kama adui zako nao wanaweza kukuwekea mipaka ili usivuke nje ya mipango yao. Mipango yao ni kuhakikisha hufanikiwi.


Ayubu 21:15 ''Sauti za utisho zi masikioni mwake; Katika kufanikiwa kwake mtekaji nyara atamjia juu yake;'' Kuna watu wametekwa nyara. Kuna watu ufahamu wao umetekwa, kuna watu uhusiano wao umetekwa na mtekaji amewawekea mipaka ili wasifanikiwe. Sifa mojawapo ya mipaka ni kwamba Yule aliyewekewa mipaka hawezi kuivuka mipaka hiyo hadi apate msaada wa kung'olewa mipaka hiyo. Nguvu pekee inayoweza kung'oa mipaka ya adui zako ni Damu ya YESU KRISTO na jina la YESU KRISTO.

Isaya 5:13 '' Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa; na watu wao wenye cheo wana njaa, na wengi wao waona kiu sana.''

Mateka huwa hawezi kuvuka mipaka ya watekaji. ikiondolewa mipaka tu kwa aliyetekwa hakika anakuwa huru. Kung'oa mipaka ni ushindi mkubwa sana.

Sijui ni jambo gani kila ukijaribu kulipata vinaibuka vikwazo.Inawezekana kabisa una mchumba wako na mnapanga kila mwaka kwamba mtaoana lakini haijawezekana huu mwaka wa 3, hamjatenda dhambi na mnadumu katika utakatifu lakini kila kitu kinagoma. ndugu mnatakiwa kung'oa mipaka yote ambayo wachawi au waganga au
watu wabaya wote wamewawekea, hakikisheni mnaiondoa mipaka hiyo kisha nyie ndio muweke mipaka kwa adui zenu, kuhakikisha hakuna adui anayeweza kuingilia mipango na baraka zenu zenu.


MCH: LAURENT
SIMU: 0762756542, 0714890889, 0782859946
 TUMA E-MAIL: mchungajilaurent@gmail.com
TUMA: WATSAP: 0762756542
subscribe youtube yetu "UPENYO WA MUNGU TV"

MUNGU AKUBARIKI SANA




Post a Comment

0 Comments