Follow us

Mpendwa katika Kristo Yesu kwanza heri ya Pasaka.

Tangazo

Ushuhuda wa Injili tunakutakia kila la heri katika kumbukumbu ya kufufuka Bwana na Mwokozi wa Ulimwengu Yesu Kristo.


Maandiko yanasema:

“Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi. Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia. Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji. Na kwa kumwogopa, wale walinzi wakatetemeka, wakawa kama wafu. Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa.


 Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema. Njoni, mpatazame mahali alipolazwa. Nanyi nendeni upesi, mkawaambie wanafunzi wake, Amefufuka katika wafu. Tazama, awatangulia kwenda Galilaya; ndiko mtakakomwona. Haya, nimekwisha waambia. Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa hofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake habari. Na tazama, Yesu akakutana nao, akisema, Salamu! Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia# Math 28:1-9. Mpendwa kufufuka kwa Bwana Yesu kulitanguliwa na ishara na nguvu za Roho Mtakatifu pale kaburini alivyoshuka kwa nguvu kubwa.


Lakini kufufuka kwa Kristo kuna maana gani kwetu?

Kwanza inatuhakikishia kufufuka kwetu tutakapokufa. Kama Kristo alivyokufa na kufufuka ndivyo nasi tutakavyokufa na kufufuka katika ufufuo wa uzima. ‘Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu,

limbuko lao waliolala’ #1Kor 15:20

Pili kufufuka kwa Kristo kumetuhakikishia sisi kuishi maisha ya ushindi ndani ya Kristo kwani Roho Mtakatifu aliyemfufua ndiye aishie ndani yetu naye atatupa kushinda dhidi ya nguvu zote za kiza. Imeandikwa ‘Lakini, ikiwa Roho yake yeye aliyemfufua Yesu katika wafu anakaa ndani yenu, yeye aliyemfufua Kristo Yesu katika wafu ataihuisha na miili yenu iliyo katika hali ya kufa, kwa Roho wake anayekaa ndani yenu’ #Rum 8:11


Na Yesu mwenyewe asema ‘Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya. Na mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi. Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa.

Mpendwa wangu tunayo nguvu sasa kwani Roho aliyemfufua Kristo yumo anaishi ndani yetu.


MUNGU AKUBARIKI SANA



Post a Comment

0 Comments