Follow us

FAHAMU MAMBO MATANO YANAYOWEZA KUZUIA AU KUCHELEWESHA MAONO NA MIPANGO YAKO

Tangazo

 


FAHAMU MAMBO MATANO YANAYOWEZA KUZUIA AU KUCHELEWESHA MAONO NA MIPANGO YAKO

1. HOFU YA KUSIMAMA PEKE YAKO.

2. KUTAKA KUELEWEKA NA KILA MTU.

3. KUTAKA KUMPENDEZA KILA MTU.

4. KUKOSA UJASIRI WA KUSEMA “HAPANA”.

5. HOFU YA KUKOSEA AU KUSHINDWA.

MFANO MZURI WA MAMBO HAYA MATANO NI YESU KRISTO:

1. Yesu Kristo alianza kazi ya kuhubiri kabla ya kuwa na mwanafunzi hata mmoja (LUKA 5:1).

- Aliaanza huduma peke yake na akamaliza peke yake (MATHAYO 26:57; MARK 14:50).

- Yesu hakuogopa kuwauliza wanafunzi wake 12 kama nao wanataka kuondoka (YOHANA 6:67).

2. Yesu Kristo hakutafuta kueleweka na kila mtu kila wakati. Wengine walimshambulia kwa nini alifanya kazi siku ya Sabato!! (MATHAYO 12:10; MARKO 3:1-6; LUKA 13:14).

3. Yesu Kristo alitaka kwanza kumpendeza Baba yake wa Mbinguni. Wakati mama yake na ndugu zake walipotaka kumtoa kwenye kusudi la maisha yake; alikataa!! (LUKA 8:19-21; YOHANA 5:19).

4. Yesu Kristo alikuwa na ujasiri wa KUKATAA kuondoka Yerusalemu sababu ya vitisho vya Mfalme Herode... akasema “HAPANA”... kamwambieni huyu ‘Mbweha’ nimekataa kuondoka!! (LUKA 13:31-32).

5. Yesu Kristo hakuwa na mawazo ya kushindwa jambo lolote. Chochote alichokusudia alikifanya, na alichokitamka kilitokea (MARKO 11:12-25).

ZINGATIA...

>>>>KABLA HUJAANZA JAMBO LOLOTE (BIASHARA, HUDUMA, MRADI, MASOMO, UJASIRIAMALI, NK), KWANZA JIULIZE, “NINAWEZA KUSIMAMA PEKE YANGU?”

>>>UKIWA NA UJASIRI WA KUSIMAMA PEKE YAKO, MUNGU ATAKULETEA WATU WA KUSIMAMA NA WEWE... HATA WAKIONDOKA UTAENDELEA KUSIMAMA‼


MAOMBI NA MAOMBEZI

PIGA 0763652896

WHATSAP 0762756542

Post a Comment

0 Comments