Tangazo
JAMBO LA KWANZA, JIFUNZE KUMTANGULIZA
MUNGU KATIKA MAMBO YAKO YOTE UNAYOTAKA KUYAFANYA AU UNAYOYAFANYA. Ukimtanguliza Mungu utakuwa tayari
kumsikia anasema nini juu ya unachokifanya kama kwa Petro na Yohana; Petro na
Yohana walimtanguliza Mungu ndio maana hata walipotishiwa kukamatwa
hawakutanguliza sababu zao binafi kwamba ‘oooh sasa ona tunaenda kufungwa’ Matendo ya Mitume 4:19 “Petro na Yohana
wakawajibu wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko
Mungu, hukumuni ninyi wenyewe”
Mtangulize Mungu wala si wanadamu, wanadamu inafikia mahali wanachoka kukusaidia
lakini Mungu hachoki. Usiwe kama Esau aliyetanguliza njaa akauza uzaliwa wake
wa kwanza. Mathayo
6:33 “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote
mtazidishiwa.”
JAMBO LA PILI, KUBALI KUANZA NA MAMBO
MADOGO: kubali kuanza mambo madogo yaliyo manyonge,
dhaifu na baadaye Mungu atakuinua. Mungu huanza na watu waliochini kabisa
wasiojua chochote na hao ndio huwatumia na baadaye huwainua na kuwapandisha
juu. Je, unataka kitu kikubwa? Kubali kuanzia chini. Iwe ni kazi kubali kuanza
na kazi hata ya chini kabisa na baadaye utaona unainuka; iwe ni biashara
usitamani hadi uanze na mtaji mkuuuubwa, hapana! Anza na mtaji wako wa kawaida
tu na Mungu atakuinua taratibu utayafikia mafanikio yako.
JAMBO LA TATU, KUBALI KUWA MVUMILIVU:Mungu hatubariki kwa sababu tunataka
tubarikiwe bali Mungu hutubariki kwa sababu ni muda muafaka wa kubarikiwa. Unamkuta
binti analalamika “yaani kwa kweli muda unaenda hata siolewi, angalia matiti
yanaanza kuning’inia” binti nakushauri vumilia tu,hayo matiti yataning’inia lakini hayawezi kudondoka, kuna
watu wanapenda matiti makubwa kama ya kwako.
Wakati mwingine usitamani mafanikio ya mwenzako kwa sababu hujui siri ya
mafanikio yake.
0 Comments