UMUHIMU WA MAOMBI YA KUFUNGA
0⃣_ Maombi kwa Mungu ni njia ya
kufikisha mahitaji yetu kwa Mungu Muumba wetu mwenye uwezo wa wa kutupatia kila
kitu tunachohitaji kwake. Maombi hufanywa na mwenye imani kuwa Mungu
yupo na kuwa atampatia hitaji lake Ebrania 11:6_
Mambo ya kufunga ni kuacha chakula cha kimwili kama njia ya kujinyima na kudhoofisha nia ya mwili na kutafuta utulivu ili useme na muumbaji wetu.
Hali hii ilianza hata kabla ya kuja kwa Yesu Kristo duniani.
Kwa mfano wanafunzi wa dini ya Kiyahudi walikuwa wanafunga mara mbili kwa wiki.
Wanafunzi wa Yohana mbatizaji pia. Lakini Yesu aliwajibu na kusema kuwa Yeye ni
Bwana arusi akiondoka tutafunga na kuomba.
KWA NINI TUTAFUNGA
1⃣. Kufunga ni sehemu ya maombi
ya kufunga.
Tunapofunga tunajinyima sehemu ya chakula na kuingia rohoni
ili kusema na Mungu kwa mambo unahitaji kwake. Unapofunga roho yako ina pata
muda wa kuwasiliana na Mungu.
*“Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika
hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba.
Luka 2:37
*Huyu mama akamwabudu Mungu kwa njia ya Kufunga na kuomba.*
Ina maana alijitoa mwili kama sadaka kwa Mungu takatifu
inayompendeza Mungu Warumi 12:1-3
2⃣ .Kufunga ni
Sehemu ya Ibada kwa Mungu
Kanisa la Mitume wakamwabudu Mungu kwa njia ya maombi ya
kufunga.
Matendo ya Mitume 13
² Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga,
Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia.
³ Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu
yao, wakawaacha waende zao.*
3 Kufunga ni
njia ya kujinyenyekeza mbele za Mungu
Mtumishi anaywafanya maombi na kufunga anapata roho ya
kunyenyekea mbele za Mungu
“Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani,
mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala
mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme,
kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.
”Esta 4:16
4⃣
Maombi ya kufunga hufanyika kama njia ya
toba kwa Mungu
“Wakakusanyika huko Mispa, wakateka maji na kuyamimina mbele
za Bwana; wakafunga siku ile, wakasema huko, Tumemfanyia Bwana dhambi. Samweli
akawaamua wana wa Israeli huko Mispa.
” 1 Samweli 7:6 (Biblia Takatifu)
5⃣ maombi ya kufunga huongeza
ukaribu na ukaribu kwa Mungu.
Lakini namna hii haitoki ila kwa kusali na kufunga.
Mathayo 17:21
MUNGU AKUBARIKI SANA KUJIFUNZA NENO HILI LA MUNGU
KWA MSAADA ZAIDI AU
MAOMBI NA MAOMBEZI
WASILIANA NA
MCHUNGAJI KIONGOZI
KUHANI LAURENT MPOMA
NCHI YA UKOMBOZI
MINISTRY
(HEMA LA MAOMBI NA
MAOMBEZI)
MWAJA KITOPE –
SINGIDA MJINI, BARABARA YA KWENDA MWANKOKO
0714890889
WHATSAP: 0762756542
0 Comments