MAOMBI YA KUKAKAMATA ANGA
Tangazo
MAOMBI YA KUKAKAMATA ANGA
Yeremia 1:8
1. Tunaingia kwa toba . omba toba
juu yako na juu ya mahali hapa omba toba juu ya kila kitu kilichopo hapa, omba
toba juu ya mji huu anga hili. Toba ni mlango wa kuingilia patakatifu. Toba ya
wazee wa kanisa hili na viongozi mbalimbali pia.
Isaya 43:25, Isaya 44:22
2. Semesha madhabahu iruhusu sauti
zetu na maombi yetu yatoke nje ya kuta za kanisa na madhabahu ili yaweze kufika
mahali tunapo taka.
1wafalme 13:1-3
3. Bomoa madhabahu za kichawi katika
mkoa huu wa Njombe, anga liachilie upenyo wa maombi, unapoomba na kubomoa
madhabahu na kufungua anga pigana mpaka ushindi upatikane
2Wafalme 11:17-20
4. Ita wakuu wa giza wanaokaa
angani, ardhini, mtoni, mtoni na hewani na kwenye misitu mikubwa na viwanja,
wanyang’anye nguvu zao na viti vyao vya enzi za kichawi hadi wakose pa kwenda.
Waefeso 6:10 – 12
5. Bomboa kuta zilizowekwa na
wachawi, kuta zenye walinzi wa kipepo piga walinzi wao wanaolinda mji kwa njia
ya kichawi, nyang’anya silaha zote kwa walinzi piga mpaka watoke kwenze malindo
yao.
Yoshua 6:5-20, Ezeliel 8:7-10
6. Wapo wa chawi wa kimataifa wanaopewa
mamlaka ya kutawala maanga mbalimbali kwaajili ya kuzuia maombi kutopenya
kwenda mbinguni au kuzuia majibu, ita malaika mikaeli asimame kupambana nao ili
kuhakikisha anga linawekwa huru kwaajili ya utukufu wa Bwana.
Mika 5:10 – 15
Nahumu 3:4. Bibi wa uchawi
7. Haribu nguvu ya giza zilizoko kwa
manefil zinazotoka kwa majini piga uwepo wao wateketeze kwa moto mpaka wapotee
8. Piga nguvu za kiganga za kichawi
vunja madhabahu ya kiganga ndani ya mkoa huu ili anga lisikile maombi yetu na
kuruhusu yapenye.
MUNGU AKUBARIKI SANA
0 Comments