JINSI YA KUBOMOA MADHABAHU ZA KISHETANIZINAZOKUTESA
Kut 34:13 “Bali utabomoa madhabahu zao, na kuvunja-vunja nguzo zao, na kuyakata-kata maashera yao.”
1. Tambua madhabahu gani zipo kwako au kwenu.
2. Tambua sababu iliyo nyuma ya uwepo wa madhabahu hizo.
3. Jitiishe kwa Mungu ili uwe salama. Hakikisha Yesu ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako!
4. Omba Mungu akupe uwezo wa kupambanua.
5. Mpinge shetani. Usiwe na urafiki na shetani. Shetani asiwe na haki fulani katika maisha yako.
6. Omba kinabii na kwa nguvu. Tambua mamlaka yako katika Bwana na kuitumia.
7. Waue makuhani wa madhabahu hizo. Tambua kwamba katika madhabahu za shetani kuna makuhani wanaohuisha maagano.
8. Jiondoe kwenye madhabahu hizo. Ondoa jina lako, picha, nguo, nembo nk kutoka kwenye madhabahu za uovu.
9. Miliki milki zako. Usisahau kuchukua kilicho halali yako. Kama madhabahu zilikuzuia kufanikiwa, sasa anza shughuli za kipato hata kama awali ulishindwa.
10. Mpe Mungu sifa. Mtukuze Mungu kwa ushindi aliokupatia.
0 Comments