Follow us

MILANGO SABA (7) AMBAYO SHETANIHUTUMIA KUINGIZA ROHO ZAKE KATIKA MAISHA YETU.

Tangazo



PASTOR LAURENT MPOMA
NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY
(HEMA LA MAOMBI NA MAOMBEZI)
MWAJA KITOPE SINGIDA MJINI.

 1. MAAGANO.

Haya ni makubaliano yaliyofanyika baina ya mtu na nguvu za giza, vizazi na nguvu za giza. Hii ni mikataba iliyofanyika na inayofanyika ambayo humpa Shetani Uhalali wa kufanya kila analotaka kufanya. Unaweza kuwa katika Agano hata bila kujua. Maarifa inahitajika kutoka chini ya maagano ya ki-shetani. HOSEA 4:6

Kuwa ndani ya Agano maana yake, “Umenunuliwa kihalali”. Pia, unaweza kuwa umeokoka ila mwili wako Shetani akawa anautumia kihalali. ITIMOTHEO 1:20

2.URITHI

Urithi unampa mtu kumiliki kihalali kitu Fulani baada ya Yule aliyekuwa anakimiliki kufariki. Kuna mambo yanatesa maisha ya watu kutokana na kuyarithi kutoka kwa watangulizi wetu yaani Wazazi, Mababu n.k. WAEBRANIA 9:16  MWANZO 25:11

Shetani ametumia nafasi hiyo kwa kupandikiza Roho zake ndani yetu baada ya wale waliokuwa na ROHO hizo kufariki au kuwa hai.

Mfano: Unamkuta mtu ni mlevi, Muhuni au mwongo sana baadaye katika uzao wake wanakuwepo watakaorithi tabia yake. Anaweza kurithi mtoto wa kwanza au mtoto mwingine.

3.NDOTO

Hii ni njia nyingine shetani anayoitumia kuingiza Roho zake kwa watu. Wengine wamejikuta wanaota ndoto mbaya kama vile kufukuzwa na nyoka, kula nyama n.k wakidhani ni jambo la kawaida lakini si hivyo maana ni njia inayoingiza nguvu za kishetani na kuyatesa maisha yetu.

Kuna aina tatu za ndoto;

i) Ndoto za Ki-Mungu 1WAFALME 3:5-12

ii)Ndoto za Ki-shetani AYUBU 4:12-21

iii)Ndoto za ki-binadamu/kawaida.

Ndoto mbaya za kishetani, Shetani huzitumia kuingizia uharibifu.

4. NDUGU

Mungu anaweza kukuadhibu kwa kosa lililofanywa na mwingine. Shetani anaweza kuingiza vifungo vyake kwako hata kama wewe haukuhusika moja kwa moja. KUTOKA 20:5

5.ENEO

Unaweza kuwa kwenye eneo linalomilikiwa na Shetani kihalali katika Ulimwengu wa giza.

Mfano: Jiulize swali, kwanini kuna sehemu zingine ukienda nguvu ya kuomba au kusoma Biblia haipo kabisa?

Shetani anapoenda Sehemu analenga Vitu Vikuu vitatu.

i) Ardhi (Lengo kuweka Ufalme wake).

ii)Miguu (Lengo kukamata nafsi ZABURI 56:6)

iii)Masikio (Lengo kuzuia usikivu)

AMOS 3:11-12

6.VITU UNAVYOTUMIA

Kuwa na mazoea ya kuombea vitu unavyotumia kwani Shetani anaweza kupitisha mapepo kwenye vitu kama nguo. Upako wa Uponyaji wa Yesu ulikuwepo mpaka kwenye nguo aliyokuwa amevaa (MATHAYO 9:20-21), Vivyo hivyo na Roho za kishetani zinaweza kuingilia kwenye nguo pia.

7.FIKRA

Shetani anaweza kuingia kwenye fikra zako ili upinge kusudi la Mungu (MATHAYO 16:23). Unaweza kuwa na Yesu lakini Shetani bado akaingia kwenye fikra zako.

MAMBO YA WALAWI 19:28


USHAURI AU UNAHITAJI MAOMBI

PIGA AU TUMA MESEJI

0714890889

WHATSAP: 0762756542

YOUTUBE: Nchi Ya Ukombozi Tv

Post a Comment

0 Comments