Tangazo
NAMNA YA KUOMBEA HALI YA
KIROHO YA ARDHI ILI UFANIKIWE KIMAISHA
LENGO : Kujifunza mbinu za kuomba ili hali
ya kiroho ya Ardhi iliyokwamisha mafanikio yako iondoke na ufanikiwe.
Kuna
uhusiano sana kati ya ardhi na mafanikio yako kwa hiyo ni muhimu sana
kulifuatilia kwa karibu sana somo hili
Tuangalie
mifano inayoonesha uhusiano wa ardhi na kufanikiwa kwa mtu.
MFANO WA KWANZA
Mwanzo
3:17-19
"Akamwambia
Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao
nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu
utakula mazao yake siku zote za maisha yako; michongoma na miiba itakuzalia,
nawe utakula mboga za kondeni; kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata
utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe,
nawe mavumbini utarudi"
Laana maana yake ni
➖Kutostawi
➖Kutofanikiwa
➖Kutokuwa na Furaha
➖Kutofikia kiwango cha mafanikio
ambacho Mungu kakikusudia kwa ajili yako. Na Laana ni kinyume cha baraka.
Mungu
aliposema ardhi imelaaniwa alikuwa anataka kumuambia Adamu kuwa ukitaka kujua
kitu gani umebeba kwa kutofuata maelekezo yangu kuwa kuna laana iliyoko kwenye
maisha yako na utakapoilima ardhi haitakuzalia matunda yake.
MFANO WA PILI
Mwanzo
4:11-12
"Basi
sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya
ndugu yako kwa mkono wako; utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa
mtoro na mtu asiye na kikao duniani."
Laana ya
hapa sura ya nne ni tofauti na ile sura ya tatu kwa sababu laana ya Adamu
ilikuwa ndani ya Adamu lakini katika sura ya nne tunaona kuwa laana ipo kwenye
ardhi moja kwa moja.Maana yake kwa kila mtu atakaye kanyaga eneo hili anapata
ile laana iliyoachiliwa kwenye ardhi .
MFANO WA TATU
2 Mambo ya
Nyakati 7:11-14
"Nikizifunga
mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu
tauni; ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na
kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka
mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao"
Uponyaji
tunaoungalia hapa ni uponyaji wa ardhi na nchi ni ardhi yenye mipaka halali ya
kiumiliki,biblia inaposema kuwa nchi maana yake ni ardhi na sio watu au taifa.
Taifa ni ni kundi la watu waliokubaliana na mfumo wa uongozi na wakae kwa
pamoja. Kwenye biblia unaona kabila linageuka kuwa Taifa au familia kuwa taifa.
(Angalia katika Kitabu cha Mwanzo 49)
Mwanzo
49:1,28
"Yakobo
akawaita wanawe, akasema, Kusanyikeni, ili niwaambie yatakayowapata siku za
mwisho.Hizo zote ndizo kabila za Israeli kumi na mbili. Na hayo ndiyo
aliyowaambia baba yao, na kuwabariki; mmoja mmoja kwa mbaraka wake
aliwabariki"
Hapa biblia
haizungumzii uponyaji wa watu bali ni ardhi .Biblia inasema tena nikiamuru
nzige kula nchi maana nzige ni wadudu waharibifu na wanaoharibu mazao au udongo
na Tauni ni ugonjwa wa kuambukiza na kibiblia ikitokea ugonjwa wa kuambukiza
ina maana kunakuwa na shida kwenye ardhi.
Ukitokea
ugonjwa wa kuambukiza katika eneo fulani huwa wanaweka karantini na kufunga
mipaka. Kitendo cha kuweka mpaka ni Roho Mtakatifu anawajulisha kuwa shida hii
imeishia mpaka hapa.
Suala hili
la kufunga mipaka ili kuzuia maambukizo ya ugonjwa ni ya kiroho kwanza kabla
hayajawa ya kimwili.
MFANO WA NNE
Yeremia
22:29-30
"Ee
nchi, nchi, nchi, lisikie neno la Bwana. Bwana asema hivi, Andikeni habari za
mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana
hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha
Daudi, na kutawala tena katika Yuda."
Huyu ni Mungu anazungumza
na nchi (ardhi yenye mipaka halali ya kiumiliki) anaposema
➖Ee nchi ,nchi sikia ---- ina maana
nchi inasikia
➖Andika maana yake inaweza tunza
kumbukumbu
➖Kuwa hatafanikiwa maana yake ni kuwa
inaweza fuatilia
Wakati
adhabu inatolewa kwa mtu huyu alikuwa bado hana watoto, lakini kumbukumbu
iliandikwa kwenye ardhi kuwa hata watoto wake wakija nao wasifanikiwe. Adhabu
ilitolewa kwa sababu gani; angalia mstari wa 21 Mimi nalisema nawe wakati wa
kufanikiwa kwako; lakini ulisema, Sitaki kusikia. Hii ndiyo iliyokuwa desturi
yako tangu ujana wako, kutokuitii sauti yangu.
Fikiria wewe
ni mtoto na umeingia kwenye adhabu ya baba au mama na unatafuta kufanikiwa na
haufaninikiwi sio kwamba akili huna bali unazo lakini umezuiliwa kufanikiwa na
ardhi kwa sababu ya kosa la baba yako na mama yako je unaombaje?
MFANO WA TANO
Mwanzo 28:
10-20
"10-13"Yakobo
akatoka Beer-sheba , kwenda harani. Akafika mahali Fulani akalala huko usiku
kucha , maana jua lilikuwa limekuchwa ,akatwaa jiwe moja la mahali pale
akaliweka chini ya kichwa chake , akalala usingizi palapale. Akaota ndoto, na
tazama ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni .Tena
tazama malaika wanapanda na kushuaka juu ya yake. Na tazama Bwana amesimama juu
yake , akasema mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahim baba yako na Mungu wa Isaka ,
nchi hii uilalayo ntakupa wewe na uzao wako"
Lile Neno
nchi hii ulalayo Kwa lugha nyingine ardhi unayolala iwe ni nyumba uliyojenga au
hoteli au umejilaza mahali kwa muda mfupi au ni kwenye basi umelala au uko
shambani umelala na ghafla unaota ndoto, sio kila mahali angeweza kulala ila
eneo lile lilikuwa na umiliki kamili wa Mungu.
MFANO WA SITA
2 Samweli
21:1
"Kulikuwa
na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu , mwaka hadi mwaka naye Daudi
akautafuta uso wa Bwana , Bwana akasema ni kwa ajili ya Sauli na nyumba yake
yenye damu kwa kuwa aliwaua hao wagibeoni"
Daudi katika
kipindi chake cha uongozi kulitokea shida ya njaa na ilidumu kwa muda wa miaka
mitatu. Na alikuwa hajaomba kutafuta sababu na alishindwa kuhusianisha kati ya
hali ya kiroho ya ardhi na shida ya njaa iliyotokea.
Kama ardhi
imekugomea jaribu kupanda mahindi na maua na baada ya muda utaona mahindi
yananyauka lakini maua yanastawi. ukimuita mtalaamu wa kilimo ataanza kupima
unyevu na atakuelekeza na sababu za kitalaam, lakini shida ni kuwa kunakuwa na
kitu kwenye ardhi ambacho hakipo sawa.
MFANO WA SABA
Ufunuo
12:12- 15
"Kwa hiyo
shangilieni; enyi mbigu ,nanyi mkaao humo ole wanchi na bahari ! kwa maana Yule
ameshuka kwenu kwenye ghadhabu nyingi akijua ya kuwa ana mda mchache tu. Na
Yule joka alipoona ametupwa katika nchi alimwudhi mwanamke Yule aliyezaa mtoto
mwanaume. Mwanamke Yule akapewa mabawa mawili ya tai Yule mkubwa ili aruke
aende zake nyikani , hata mahali pake, hapo alishwapo kwa wakati na nyakati na
nusu ya wakati mbali na nyoka huyo,Nyoka akatoa katika kinywa chake nyuma ya
huyo mwanamke maji kama moto amfanye kuchukuliwa na mto ule"
Huyu mama
angejuaje kuwa kufanikiwa kwake kulitegema sana msaada wa ardhi ambayo uliumeza
mto uliotolewa na Joka. Kwa hiyo hakikisha kila ardhi iko upande wako, iwe ni
ya kanisa au unapolala au unapofanya biashara.
kwenye
semina zetu kuwa tunahakikisha mbingu na ardhi inakaa upande wetu ili kumzuia
shetani.
Sasa
hujiulizi kwanini kambi nyingine huwa wanachimbia hiziri ardhini?. Jibu ni
rahisi kabisa kuwa wanataka msaada wa ardhi
Kwani
wanapofanya mambo ya mila wanapoweka maziwa mdomoni na kuweka na kutemea juu na
chini kwenye ardhi wanakuwa wanatafuta nini, wanatafuta msaada wa mbingu na
nchi.
MFANO WA NANE
Yoel 1:9-13
"Sadaka
ya unga na sadaka ya kinywaji Zimekatiliwa mbali na nyumba ya Bwana; Hao
makuhani, wahudumu wa Bwana, wanaomboleza. Shamba limeharibika, nchi
inaomboleza; maana nafaka imeharibika, divai mpya imekauka, mafuta yamepunguka.
Tahayarini, enyi wakulima; Pigeni yowe, enyi watunzaji wa mizabibu; Kwa ajili
ya ngano na shayiri, Maana mavuno ya mashamba yamepotea. Mzabibu umesinyaa,
mtini nao umevia; Nao mkomamanga na mtende na mtofaa; Naam, miti yote ya
mashamba imekauka; Maana furaha imekauka katika wanadamu. Jikazeni mkaomboleze,
enyi makuhani; Pigeni yowe, enyi wahudumu wa madhabahu; Njoni mlale usiku kucha
katika magunia, Enyi wahudumu wa Mungu wangu; Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka
ya kinywaji Zimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu"
Unaombaje
ikiwa hali ya kiroho ya ardhi imesababisha kuzuiwa kwa sadaka kanisani. Mungu
kakataza sadaka ili waombaji waombe ili hali zao za Uchumi ziwe vizuri na watoe
sadaka.
Na kama
unafanya semina au mkutano wa nje kama sisi usipojua namna ya kuombea ardhi
utakuta watu wanarudi na sadaka nyumbani kwao kwa sababu hali ya kiroho ya
ardhi ina uhusiano mkubwa sana na utoaji wa sadaka kwa watu
MFANO WA TISA
Kumbukumbu
la torati 8:7,12
"Kwa
kuwa Bwana, Mungu wako, yuakuingiza katika nchi nzuri, nchi yenye vijito vya
maji, na chemchemi, na visima, vibubujikavyo katika mabonde na milima; Angalia,
utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani
yake;"
Kuna
uhusianio na Baraka za Mungu na watu waliongizwa kwenye eneo lenye mipaka
halali ya kiumiliki. Ndio maana kati ya adhabu mojawapo inaifikia nchi ni miji
kubomolewa au kukosa wakazi, kuwa ukiwa.
Sasa unaweza
jiuliza swali hili gumu kuwa kwanini Sauli hakupata adhabu yeye katika kipindi
chake baada ya kuwaua wagebeoni. Lakini aliyepata madhara ni Daudi, kwa hiyo si
tu kwamba Daudi alirithi kiti bali na ile adhabu iliyokuwa kwenye kiti. Pia
kuna uhusiano gani uliopo kati ya ardhi na cheo kosa la kiti na kosa la mtu
aliyekaa kwenye kiti na kosa la kiti.
Kosa la kiti
adhabu yake atapata kila mtu atakayekaa kwenye kiti, kwa hiyo kumfukuza kwa
jinsi ya mwili kwa sababu amekosea haitatui tatizo la kiroho lililofanya
akakose mtu mwingine atakayekuja atajikwaa palepale alipojikwaa wa kwanza.
MUNGU AKUBARIKI SANA
MAOMBI NA MAOMBEZI
0 Comments