MAMBO YANAYOTOKEA UKIISHI KATIKA
MAOMBI
Nguvu na
Matokeo Makubwa Kwenye Maombi haipo Kwenye KUOMBA Bali NIDHAMU KUBWA KATIKA
KUOMBA KWA MWENDELEZO
Kwa sababu
Kanuni Mojawapo inayosababisha Na Kuleta Matokeo Makubwa Kwenye Maombi ni
NIDHAMU ALIYONAYO MTU YA KUOMBA KWA MWENDELEZO
Sasa nataka
tuangalie kidogo Mambo kadhaa Yanayotokea Pale Mtu anapoishi Maisha Ya Maombi
Kwa MWENDELEZO
(1) MAISHA YA MAOMBI HUSABABISHA MTU APATE MAJIBU YAKE KUTOKA KWA
BWANA
Luka 11:8
[8]Nawaambia
ya kwamba, ijapokuwa haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile
asivyoacha kumwomba, ataondoka na kumpa kadiri ya haja yake.
Hakuna Namna
ambavyo utaishi Maisha Ya Maombi Kwa MWENDELEZO halafu usipate Majibu Yako
Kutoka Kwa MUNGU Kwa Yale ambayo unayaombea
Unapokuwa na
Maisha Ya MWENDELEZO Katika Maombi ni lazima tu utakuwa ni Mtu mwenye kujibiwa
na BWANA
(2) MAISHA YA MAOMBI HUSABABISHA
UWEPO WA MUNGU KUYAZINGIRA MAISHA YAKO
Zaburi 91:1
[1]Aketiye
mahali pa siri pake Aliye juu
Atakaa
katika uvuli wake Mwenyezi.
Hakuna namna
ambavyo utaishi Maisha Ya Maombi Kwa MWENDELEZO halafu Uwepo Wa MUNGU Usiwe
Pamoja nawe
Hakuna namna
ambavyo utaishi Maisha Ya Maombi Kwa MWENDELEZO halafu Uwepo Wa MUNGU Usiwe
halisi Kwenye Maisha Yako
Maana
unapokuwa na Nidhamu Kubwa kuhakikisha Kila Siku ,Kila Siku unakuwa na Muda
mwingi Sana Wa KUOMBA hiyo hali Huwa inatengeza Uwepo Wa MUNGU Kuwa Halisi na
Kuyazingira Maisha Yako
(3) MAISHA YA MAOMBI HUSABABISHA USHINDI
HAIJALISHI UTAKUTANA NA NINI
Kama
nilivyosema Kwenye point namba 2 Kuwa Ukiishi Maisha Ya Maombi Kwa MWENDELEZO
Huwa Uwepo Wa MUNGU unakuwa nawe
Sasa huo
Uwepo Wa MUNGU Huwa unasababisha Upate Ushindi Haijalishi utakutana na Nini ,
Haijalishi utasongwa na Nini
Aaah
kilichompa Ushindi Daniel Kwenye tundu la simba ni ILE NIDHAMU KUBWA ALIYOKUWA
NAYO YA KUOMBA KWA MWENDELEZO
Daniel
alikuwa anaomba mara 3 Kwa Siku Kila Siku,Kila Siku Haijalishi Yuko busy namna
gani
Ndugu Yangu
Ukiishi Maisha Ya Maombi Kwa MWENDELEZO Haijalishi vita gani ambazo
zinawaangusha Wengine Wewe haitakuangusha Kamwe , Haijalishi Majaribu na
Changamoto Gani zitakuja mbele Yako ni lazima tu UTAZISHINDA
DANIEL 6:10 , WARUMI 8:37
(4) MAISHA YA MAOMBI HUSABABISHA UWE
MBABE KWA SHETANI NA MAWAKALA WAKE
Kamwe Huwezi
Kuwa mbabe Kwa Shetani kama hauishi Maisha Ya Maombi
Kamwe
hauwezi Kuwa mbabe Kwa Shetani kama una Maombi Ya mara Leo umeomba, Kesho
hauombi
Lakini
Ukiishi Maisha Ya Maombi Kwa MWENDELEZO Kwa Muda mrefu aah lazima Nguvu za Giza
zitakuogopa , lazima Nguvu za Giza zitakukimbia
Maana
utakuwa umezungwa na Uwepo na Utukufu Mwingi Wa MUNGU
(5) MAISHA YA MAOMBI HUSABABISHA
KUISHI MAISHA MBALI NA HOFU ,MASHAKA , WOGA
Ukiishi
Maisha Ya Maombi Kwa MWENDELEZO unatengeneza Uwepo Wa MUNGU Kuwa nawe
Na ule Uwepo
Wa MUNGU unasababisha Uwe na ujasiri usiyo Wa kawaida, unasababisha Uwe na
Imani isiyo Ya Kawaida
Na Hofu,
mashaka, wasiwasi, woga vinakuwa mbali nawe
2 Timotheo 1:7
[7]Maana
Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Huwezi
kukuta Mtu anayeishi Maisha Ya Maombi Kwa MWENDELEZO halafu akawa mwoga mwoga ,
halafu akawa na mashaka mashaka , Halafu Hofu zikamtawala
(6) MAISHA YA MAOMBI HUSABABISHA
USHINDI DHIDI YA KILA DHAMBI
Hakuna
Dhambi Yenye Nguvu Ya kumtawala ,kumuendesha Mtu anayeishi Maisha Ya Maombi Ya
MWENDELEZO
MUNGU AKUBARIKI SANA KUFUATILIA BLOG
HII
NAITWA MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY
(HEMA LA MAOMBI NA MAOMBEZI)
KWA MAHITAJI PIGA AU TUMA UJUMBE HAPA
0714890889
WHATSAP: 07627576542
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
TUMA MAHITAJI YAKO KWA NAMBA HAPO
JUU.
UNAWEZA KUCHANGIA SADAKA YAKO KWA
AJILI YA UJENZI WA KANISA KATIKA VITU VIFUATAVYO:
1. VITI 20 @ 20,000/=
2. MAIKI 2= 150,000/=
3. ENEO LA KANISA 500,000/=
4. SIKA 2 = 1900,000/=
5. VITAMBAA VYA MADHABAHU.= 100,000/=
TIGO PESA:
+255714890889................JINA: LAURENT MPOMA
M-PESA:
+255762756542.....................JINA: LAURENT MPOMA
AIRTEL MONEY:
+255782859946.........JINA: LAURENT MPOMA
MCHUNGAJI ATAKUOMBEA .
MUNGU AKUBARIKI SANA WEWE
UNAYECHANGIA KWA AJILI YA MUNGU NA AKUFUNGULIE MALANGO YAKO YA UCHUMI.
0 Comments