Follow us

SOMO: YATAZAME MAMBO KUTOKEA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO ILI UFANIKIWE

Tangazo

 

MCHUNGAJI LAURENT MPOMA

YATAZAME MAMBO KUTOKEA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO ILI UFANIKIWE

Katika 2 Wafalme 6:15-17 imeandikwa ‘Hata asubuhi na mapema mtumishi wake yule mtu wa Mungu alipoondoka, na kwenda nje, kumbe! Pana jeshi la watu, na farasi na magari, wameuzingira mji ule. Mtumishi wake akamwambia, Ole wetu! Bwana wangu, tufanyeje? Akamjibu, USIOGOPE; maana WALIO PAMOJA NASI ni wengi kuliko wale walio pamoja nao. Elisha akaomba, akasema, Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote’.

Kuna tofauti kubwa sana ya kuyatazama mambo kwa macho ya mwili na kuyatazama kwa macho ya kiroho. Ndio, ipo tofauti ya kuona mambo kutokea kwenye ufalme wa nuru na kuyaona kutokea kwenye ufalme wa giza. Tambua kuwa kila hatua au changamoto unayoipitia, namna ulimwengu wa roho wanavyoitazama ni tofauti na ulimwengu wa mwili wanavyoitazama. Hivyo basi watoto wa Mungu wanapaswa wajifunze kuyatazama mambo kutokea kwenye ulimwengu wa roho kwa macho ya ufalme wa nuru ili wafanikiwe.

JE, ULIMWENGU WA ROHO NI NINI? – Biblia kwenye kitabu cha Waefeso 1:3 na Waefeso 6:10-12 imeeleza kuhusu uwepo na uhalisia wa ulimwengu wa roho kama ilivyo kw ahabari ya ulimwengu wa mwili. Ulimwengu wa roho ni makazi ya ufalme wa Mungu na ufalme wa Shetani, kila ufalme ukiwa na eneo lake la utawala ingawa Mungu au viumbe wa ufalme wa nuru wana uwezo wa kuingia na kutoka eneo la ufalme wa giza ikiwa kuna kusudi la kwenda huko.

 

Ulimwengu wa roho  ni makazi ya roho zisizo na mwili wa damu na nyama na huko kuna viumbe mbalimbali vya kila ufalme ambapo Malaika ndio watendaji wakuu kwenye ufalme wa nuru na Mapepo ndio watendaji wakuu kwenye ufalme wa giza. Falme hizi mbili zinafanya kazi kwenye ulimwengu wa mwili kutokea kwenye ulimwengu wa roho, kwa sababu wao ni roho  zisizo na mwili huu wa damu na nyama (Yohana 4:24 na Waefeso 2:2).

KWA NINI KUYATAZAMA MAMBO KUTOKEA KWENYE ULIMWENGU WA ROHO?

·         Neno la Mungu ndio sheria inayotawala kwenye ulimwengu wa roho. Neno ndio linaloufungua na kuufunua ulimwengu wa roho kwenye roho ya mtu. Hivyo ni wajibu wa mtu kulisoma na kulitafakari neno kila siku ili kuona kilichomo ndani yake. Ndio, Mungu anatatarajia watoto wake waweze kuona mambo kwa kulisoma neno lake, naam wasome na kuwaza mpaka waone kilichobebwa kwenye neno (Yeremia 1:11-12, Warumi 8:1-2, Mathayo 7:21-23, Ufunuo wa Yohana 12:17).

·         Matokeo na uhalisia wa jambo kwenye ulimwengu wa mwili unaanzia na unategemea utendaji wa mtu kwenye ulimwengu wa roho. Chochote kinachotokea duniani kimefanyika kwanza kwenye ulimwengu wa roho. Maamuzi anayofanya mtu kwenye ulimwengu wa roho ndio yanayoamua hali na hatma yake kwenye ulimwengu wa mwili. Tambua, watoto wa Mungu wana mamlaka ya kuamua namna wanavyotaka mambo yawe kwenye ulimwengu wa mwili  kwa kutumia nafasi zao za ulimwengu wa roho. Rejea Isaya 62:-7, 1 Wakorintho 2:8-9. (Isaya 62:6-7, Danieli 4:13-17, Danieli 10:11-13, 2Wakorintho 10:3-5).

·         Kuona ndio msingi wa kufanikiwa katika kuviga vita vya kiroho – Kuyatazama mambo kutokea kwenye ulimwengu wa roho ni moja ya mbinu za kumsaidia mwamini katika kuvipiga vita vya kiroho na kushinda. Kushindwa au anguko la wakristo wengi leo ni matokeo ya kutokujua namna ya kuvipiga vita vya kiroho. Hivyo kuwa na uwezo wa kuona mambo kutokea kwenye ulimwengu wa roho ni muhimu sana na tena ufunguo wa ushindi (2 Wafalme 6:8-11)

MUNGU AKUBARIKI SANA KUJIFUNZA MANENO YA MUNGU

MAOMBI NA MAOMBEZI

WASILIANA NA MCHUNGAJI LAURENT MPOMA

NCHI YA UKOMBOZI MINISTRY

(HEMA LA MAOMBI NA MAOMBEZI)

PHONE: +255714890889

WHATSAP: +255762756542

TUMA MAHITAJI YAKO LEO MCHUNGAJI ATAKUOMBEA NA KUKUPATIA USHAURI.

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

SOMA : (2 MAMBO YA NYAKATI 1:7:  Usiku ule Mungu akamtokea sulemani, akamwambia, omba utakalo nikupe).

Tunaupanuzi wa kiwanja cha kanisa ambacho kinahitaji shilingi milioni tatu (3,000,000/=). Kiasi chochote tunapokea. MUNGU akubariki sana kwa utoaji wako. Hakika Amini Mungu anakwenda kukutana na wewe kama sulemani alivyotokewa usiku ule sasa ni zamu yako.

UNAWEZA KUTUMA HAPA

MPESA: +255762756542……………..JINA: LAURENT MPOMA

TIGO PESA: +255714890889…………JINA: LAURENT MPOMA

AIRTEL MONEY: +255782859946…….JINA :LAURENT MPOMA

CRDB BANK: 0152363022800………LAURENT ELIAS MPOMA

NMB BANK: 50810025078……..LAURENT ELIAS MPOMA

JJ


Post a Comment

0 Comments