KUJITOA KWENYE VIFUNGO VYA MANENO
MABAYA
4 Je!
Umetamka maneno kwa nani? Kisha ni roho ya nani iliyotoka kwako?
Ayubu 26 :4
Neno lolote
ulilotamkiwa ni roho
Kama neno
hilo ni roho basi ujue kuwa unenewa linafanya kazi maishani mwako sawasawa na
lilivyotamkwa.
kwa kuwa
neno ni roho , neno lolote baya ulilotamkiwa ujue linakamata mfumo mzima wa
maisha yako .
Tambua kuwa
neno baya ukitamkiwa ile roho ya uharibifu inakuja kwako kukukamata.
Ukitamkiwa
kutokufanikiwa huwezi kufanikiwa kweli kama hujalitubia hilo neno na kulikata
lisikukamate .
2 Basi umetegwa kwa maneno ya kinywa
chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako,
Mithali 6 :2
Maneno yanakamata na pia yanashika
Neno lolote
la kushindwa ukitamkiwa kama anayekutamkia unamsikia mkanye hapo hapo mwambie
maneno yake hayatasimama usipofanya hivo yatathibitika kwako
Kama
ulitamkiwa na mtu hutakaa uoe au hutakaa uolewe tambua kuwa unanafasi ya kutubu
juu ya maneno hayo na kuyafuta kabisa yasifuatilie maisha yako
Kuna wakati
unaweza kuona kuwa mume uliyenaye au mke uliye naye siyo sahihi kwako kumbe
kuna mtu alikutamkia kuwa hutakaa kwenye ndoa yako ukaifurahia .
Ndoa nyingi zinaingia migogoro kwa sababu ya
maneno mabaya yaliyotamkwa juu yake .
29 Ee nchi, nchi, nchi, lisikie neno la Bwana.
Yeremia 22 :29
30 Bwana
asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu
hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake
atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena
katika Yuda.
Yeremia 22 :30
Itazame hiyo familia imetamkiwa
kutokufanikiwa kabisa
Utaona ardhi
( nchi) imetekeleza yale matamko na kuwafanya watu wakaao hapo kutokufanikiwa
kabisa .
Lazima
uyafute maneno yote mabaya uliyotamkiwa na watu kwa kusikia na kwa kutokusikia
.
Ninakwambia
ujifungue utoke kwenye vifungo vya maneno nikimaanisha kuwa neno lolote ukitamkiwa ujue linaumba .
1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu
na nchi.
Mwanzo 1 :1
2 Nayo nchi
ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji;
Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
Mwanzo 1 :2
3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa
nuru.
Mwanzo 1 :3
Tambua kuwa
Mungu aliumba vitu vyote kwa neno
1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno
alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
Yohana 1 :1
2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
Yohana 1 :2
3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala
pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
Yohana 1 :3
4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima,
nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
Yohana 1 :4
5 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza
halikuiweza.
Yohana 1 :5
Kwa maana
hii basi mtu akikutamkia neno litakuwa sehemu ya maisha yako usipolifuta kwa
maombi( toba ).
9 Maana Yeye alisema, ikawa; Na Yeye
aliamuru, ikasimama.
Zaburi 33 :9
10 Bwana huyabatilisha mashauri ya
mataifa, Huyatangua makusudi ya watu.
Zaburi 33 :10
Neno lolote
ukijitamkia au kutamkiwa linasimama juu yako
Ukijitamkia
kushindwa utashindwa kweli kweli .
Bwana Yesu ,
ninakuja mbele zako .
Ninakuomba
unisamehe maana nimejitamkia maneno mabaya ya kushindwa.
Nirehemu ee
BWANA , maana sikukujua lakini sasa nimejua makosa yangu juu ya maneno mabaya
niliyojitamkia.
Nakuomba
uyafute maneno mabaya niliyojitamkia katika maisha yangu , katika jina la Yesu
.
Ninaomba
uwasamehe hata wale walionitamkia maneno mabaya juu ya familia yangu , biashara
zangu, ndoa yangu , elimu yangu n.k
Ee Mungu
uyafute maneno yao mabaya , waliyonitamkia kwa kujua na kwa kutokujua. Kwa damu
ya Yesu futa maneno yao kuanzia sasa , maana imeandikwa:
10 Bwana huyabatilisha mashauri ya
mataifa, Huyatangua makusudi ya watu.
Zaburi 33 :10
11 Shauri la Bwana lasimama milele,
Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi.
Zaburi 33 :11
Nami
nakuomba maneno niliyotamkiwa uyafutilie mbali katika maisha yangu , familia
yangu , ndoa yangu n.k bali neno lako likasimame daima maishani mwangu katika
jina la Yesu .Amen
Katika jina
la Yesu , ninasema kama ilivyoandikwa;
7 Bwana MUNGU asema hivi, Neno hili
halitasimama wala halitakuwa.
Isaya 7 :7
Ninaamuru
kila maneno mabaya kutokusimama katika maisha yangu na ndoa yangu , familia
yangu , elimu yangu n.k
10. Fanyeni shauri pamoja, nalo
litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.
Isaya 8 :10
ninayaamuru
maneno yote mabaya niliyotamkiwa na niliyotamkiwa kuwa batili , katika jina la
Yesu.
Ninaamuru
kila maneno mabaya na roho ya uharibifu kuachia maisha yangu , katika jina la
Yesu nina yavua mavazi ya maneno mabaya kwa damu ya Yesu .
22 Na katika Torati karibu vitu vyote
husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga damu hakuna ondoleo.
Waebrania 9 :22
Asante Bwana
Yesu kwa kuwa unasikia kuomba kwangu nami najikabidhi mikononi mwako sasa na
hata milele .Amen
MUNGU AKUBARIKI SANA KWA KUENDELEA
KUFUATILIA BLOG HII NA KUJIFUNZA ZAIDI.
MAOMBI NA MAOMBEZI
WASILIANA NA MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
PIGA 0762756542
WHATSAP: +255762756542

0 Comments