VIFUNGO VYA
MWILINI
Utangulizi:
Mungu
anawapenda sana wanadamu na Biblia inasema wazi kuhusu hili katika kitabu cha
Maombolezo 3:31; Ni raha yake kuona hatuna matatizo na tunaishi kwa amani.
Mungu hakumuumba mwanadamu ateseke bali alimuumba afanikiwe akiwa duniani na
kuishi kwa furaha.
Wakati
huohuo, shetani kwa asili hapendi mtu aliyeumbwa na Mungu afanikiwe na ndio
maana katika Luka 3:16 inasema, “…ambaye shetani amemfunga miaka kumi na
minane…” (Matendo 10:38; 2Wathesalonike 2:18-19) kwa maandiko hayo tunaweza
kujua kuwa shetani anaweza kufunga, kuzuia, kupinga na kushindana na mtu.
Kwa asili
shetani ni mshindani na furaha yake ni kuwatesa wanadamu ambao wanapendwa na
Mungu. Yeye hufanya hivi ili kuumiza moyo wa Mungu kupitia wanadamu walioumbwa
na Mungu.
SHETANI
ANAWEZA KUMFUNGA MTU:
Kama
tulivyoona kuwa shetani anapenda kuwatesa wanadamu na ili kutimiza lengo lake
njia mojawapo anayotumia ni kuwafunga watu. Na tunapotaja vifungo, tunakuwa
tunazungumzia vifungo vya aina kuu tatu, yaani, Vifungo vya mwilini, Vifungo
vya rohoni na vifungo vya nafsini kwasababu mtu ni roho inayokaa ndani ya
nyumba iitwayo mwili. Katika hatua hii ya kwanza tunaanza kuangalia kwa undani
kuhusu vifungo vya mwilini:-
Mwili ni
nini?
Hatuwezi
kujua namna mwili unavyoweza kufungwa bila kujua asili ya mwili wa binadamu.
Tuanze kwa kuangalia andiko hili Mwanzo 2:7 “BWANA Mungu akamfanya mtu kutoka
katika mavumbi ya ardhi…” kumbe asili ya mwili wa mwanadamu ni mavumbi au
udongo. Na ndio maana katika Isaya 64:8 Biblia inasema, “… sisi tu udongo nawe
ni mfinyanzi wetu...” nabii Isaya ambaye aliwahi kumuona Mungu lakini alijua
ukweli huu kuwa mwili ni mavumbi (Ayubu 7:21, 34:15). Kumbe pamoja na kuwa
umevaa vizuri au umeupamba mwili vizuri lakini asili yake ni udongo na katika
ulimwengu wa roho huonekana kuwa ni udongo kabisa. Kwa ufupi mwili wa mwanadamu
ni udongo na mtu anapokufa mwili huirudia nchi (Mhubiri 12:7) yaani mavumbi.
Ndio maana
hata watu wanapooana ni miili ndio ambayo inakuwa imeoana na si roho kwasababu
mbinguni hakuna kuoa wala kuoana kule ni katika roho. Kwa kujua kuwa mwili ni
udongo basi namna ambayo unaweza kuutendea udongo wa kawaida ndivyo vilevile
waweza kuutendea mwili wa binadamu. Udongo wa ardhini waweza kuoteshwa mimea na
kuchimbwa, vilevile na mwili wa binadamu waweza kufanyiwa hivyo.
TOFAUTI KATI
YA MWILI NA UDONGO WA KAWAIDA:
Kuna mambo
mawili makuu yanayosababisha mwili wa binadamu uwe tofauti na udongo wa kawaida.
1. Mwili
uliwahi kushikwa na mikono ya Mungu maana hakuna kitu kilichowahi kushikwa na
Mungu na kikabaki kama kilivyo.
2. Ndani ya
mwili wa mwanadamu kuna roho ambayo huuisha mwili na kuupa uhai. Kwasababu hizo
mwili wa mwanadamu hutofautina na udongo wa kawaida.
MWILI WA
MWANADAMU UNAWEZA KUPANDIWA VITU:
Biblia iko
wazi kuwa Mungu wa mbinguni anaweza kupanda, (Mwanzo 2:8); kumbe Mungu ambaye
ni roho (Yohana 4:24) anaweza kupanda katika ardhi kabisa vivyo hivyo shetani
naye ni roho naye ana uwezo wa kupanda katika mwili ambao kwa asili ni udongo.
Hapa ndipo lile andiko la “KILA PANDO AMBALO BABA WA MBINGUNI HAKULIPANDA LITANG’OLEWA”
linapoleta maana; Mapando ambayo hayajapandwa na Baba wa mbinguni ni lazima
yatakuwa yamepandwa na shetani. Ndio maana ya mfano wa Yesu katika Mathayo
13:25 “lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya
ngano, akaenda zake.” Huyo ambaye Yesu anamwita adui ni shetani mwenyewe. Kumbe
unapolala au kujisahau shetani huja na kupanda magugu, hili jambo linatendeka
katika ulimwengu wa roho. Ni muhimu kujua siri hii kwamba kama vile udongo
unavyopandwa vivyohivyo shetani naye anao uwezo wa kupanda juu ya mwili wa
mwanadamu.
Unaweza
kumsikia mtu analalamika kuwa mwili unachoma lakini kumbe katika ulimwengu wa
roho mtu huyo amechomwa mkuki au kisu. Kufikia hapa sasa twaweza kujua kwanini
Mungu alikataza kupanda mbegu mbili za tofauti katika shamba moja (Mambo ya
Walawi 19:19). Mungu alisema hivi akitufundisha kuwa mahali ambapo Mungu
amepanda shetani hatakiwi kupanda mahali pale. Mtu anaweza kuhisi vitu
vinatembea mwilini kumbe amepandiwa wanyama wanaotembea katika mwili wake.
PEPO ANAWEZA
KUJIGEUZA NA KUWA CHOCHOTE:
Tulijifunza
kuhusu sheria mbili za rohoni, hapo tuliona uwezo wa pepo wachafu kujigeuza na
kuwa kitu kingine yaani kuvaa sura mbali mbali ili kutimiza kazi zao. Jambo
hili twaweza kuliona katika (1Wafalme 22:19-23) huyu pepo kwa asili hakuwa wa
uongo lakini aliweza akaenda na akawa pepo wa uongo. Yule pepo akaingia katika
vinywa vya manabii wa Mfalme Ahabu na kuwafanya wamtabirie uongo. Kwa maana
hiyo tunaona uwezekano wa pepo mchafu kujigeuza na kuwa kitu chochote ili
kutimiza lengo alilokusudia.
Sasa twaweza
jua kuwa mapando tuliyokuwa tunayazungumzia ni pepo wachafu ambao hujigeuza na
kuwa kile kitu na hivi ndivyo vinavyoitwa “Vifungo vya mwilini”. Wakati
mwingine pepo anaweza kujigeuza na kuwa kinywa cha mtu, kama pepo wa katika
(1wafalme 22:19-23) alivyofanya. Hivyo; unaweza kumuona mtu anatukana matusi ya
ajabu bila hata aibu, kumbe pepo kajigeuza na kuwa kinywa chake. Pepo anaweza
kuwa uso wa simba, unamkuta baba mwenye nyumba mkali kwa watoto na mkewe kumbe ni
uso wa simba. Kwahiyo; pepo wanaweza kujigeuza maumbo mbalimbali kama nyani,
simba, paka hata bundi ili mradi kuharibu hatma ya mtu. Mnamkuta dada aolewi
kumbe uso wake umefunikwa kwa sura ya simba, kila mwanaume anayetaka kumchumbia
haoni sura nzuri bali anaona simba. Na ndio maana kuna baadhi ya wadada watumia
muda mwingi kujipodoa lakini bado hawapendezi kwa kuwa uso sio wa kwake.
KUNG’OA KILA
KILICHOPANDWA KATIKA MWILI WAKO:
Imeandikwa
kila pando asilolipanda Baba wa mbinguni litang’olewa, hivyo Mungu ametupa
mamlaka ya kung’oa kila pando la kishetani yaliyopandwa katika mwili. Miili
yetu ni Hekalu la Roho Mtakatifu hivyo shetani hatakiwi kugusa sehemu yoyote ya
mwili wako.
Tumia
mamlaka yako kung’oa kila pando ambalo shetani amepanda katika maisha yako
mapando ya magonjwa, homa zisizoisha, ukimwi, mwasho wa mwili na matatizo
mbalimbali. Jina la Yesu lina mamlaka yote dhidi ya kazi zote za shetani katika
maisha yako.
MAOMBI NA
MAOMBEZI
WASILIANA NA
MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
KANISA LA
ELIM PENTEKOSTE (NCHI YA UKOMBOZI) – MWAJA KITOPE SINGIDA MJINI
SIMU:
0762756542
WHATSAP:
0762756542
YOUTUBE:
Upenyo Wa Mungu Tv

0 Comments