1. IMARISHA FAHAMU YA IMANI
–Pasipo Imani haiwezekani kumpendeza Mungu, Imani ni kutokuwa na mashaka akilini mwako. Zaidi ya milango mitano ya fahamu yaani kuona, kunusa, kuonja, kusikia na kuhisi LAKINI Imani ni mlango wa sita (Japokuwa kwangu Mimi Gustaph ni wakwanza). Maisha yakijawa na Imani kwa kila jambo unalofanya huwezi kukwama.. 2Petro 1:5-8
“Kwa sababu hii, jitahidini sana kuongeza wema katika imani
yenu; na katika wema ongezeni maarifa;
na katika maarifa ongezeni kiasi; na katika kiasi ongezeni ustahimilivu;
na katika ustahimilivu ongezeni kumcha Mungu;
na katika kumcha Mungu ongezeni upendano wa kindugu; na katika upendano
wa kindugu ongezeni upendo. Maana mkiwa
na sifa hizi kwa wingi zitawawe zesha kuwa wenye bidii na wenye kuzaa matunda
katika kumfahamu Bwana wetu Yesu Kristo.
-katika Imani yenu tieni na WEMA, wewe amua kuweka wema
maana hii ni kazi yako, usiseme Mimi ndivyo nilivyo, KATAA UBAYA
2. JIHESABU KAMA MUNGU ANAVYOKUHESABU.
Hapo sasa ni kuweka nia ya Kristo katika MWENDO. Wafilipi
4:13 ”Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu”.
-Umekubali kutembea kandokando ya mto, basi utakutana na
bahari unayohitaji. Nia yako lazima iungwe mkono kwa vitendo. Kutokuruhusu nia
itafsiriwe kwa vitendo ndiko kunakomtofautisha mtu anayefanikiwa na ambaye
hafanikiwi. Wengi wakiruhusu matendo yao
yafunue nia zao za kufànikiwa watakuwa na maendeleo makubwa.
3. BATILISHA FIKRA ZA KITOTO NA UAMUE KUKUA.
1wakorinto 13:11 “Nilipokuwa mtoto mchanga, nilisema kama
mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga,
tokea hapa nilipokuwa mtu mzima; nimeyabatilisha mambo ya kitoto”.
Paulo anasema alipokuwa sasa, yaani tokea amekuwa mtu mzima
amebatilisha fikra za kitoto. Maana ya kubatilisha ni kukichukua kitu na
kukiweka pembeni kwa lengo la kutokukitumia tena, kimekuwa batili ina maana
hakiruhusiwi kutumika tena na inatakiwa sasa hapo kikae mbali kidogo.
1Wakorinto 14:20
”Ndugu zangu, msiwe watoto katika akili zenu, lakini katika uovu mgeuzwe
watoto wachanga, Bali katika akili zenu mkawe watu wazima”. -Utoto unaozungumziwa hapa ni utoto wa akili,
soma Waefeso 4:14.
4. USIKATAE FURSA ZA KUWA MDOGO.
Mathayo 20:26-27 “Lakini haitakuwa hivyo kwenu, bali mtu
yeyote anayetaka kuwa mkubwa kwenu na awe mtumishi wenu; Na mtu yeyote
anayetaka kuwa wa Kwanza kwenu na awe mtumwa wenu”.
-Anza kuwatumikia wengine kwanza, anza kuwapatia MEMA
wanayopenda kwanza na utakuwa umewatawala bila wao kujijua. Angalia wafalme
walivyojishusha na walivyofanikiwa, mfano Yesu Kristo.
5. UNALOTAKA UTENDEWE WATENDEE KWANZA WENGINE.
Mathayo 7:12 ” Basi yoyote mtakayo mtendewe na watu, nanyi
watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii”.
–Mara nyingi watu WEMA wanabeba mizigo mingi kupita kawaida,
kubali kufunua hekima zako kupitia uvumilivu ili uwavute waamini unachoelewa.
Au yafaa nini mwanadamu unapenda kuheshimiwa halafu wewe huheshimu wenzako?
“DAWA YA MOTO NI MAJI”, kwanini ubebe moto kifuani mwako ili
uzime moto uliowashwa na mwenzako?.
6. FANYA JAMBO ZURI UNALOLIHOFU.
Hofu na mashaka ni silaha kubwa sana ambayo shetani huitumia
kuwafanya watu washindwe kupata majibu ya maombi ya miujiza yao kutoka kwa
MUNGU. Shetani anafahamu kwamba imeandikwa;
” Mwenye haki wangu ataishi kwa imani, naye akisitasita Roho
yangu haina furaha naye” (Waebrania 10:38).
Dawa kubwa ya hofu ni Imani (Marko 11:22). Unapohofia baya
usilolihitaji ni ushindani kati ya mwili na imani, iite roho; inajua hilo ni
baya, mwili unadai ni zuri. Thibitisha kuwa ni baya kwa kuliacha. Aina za hofu
ni pamoja na kukosolewa, kuchekwa, umaskini, kufilisika, kuachishwa
kazi,kustaafu, kufiwa n.k
7. IMARISHA UNYOOFU WAKO/UAMINIFU.
Ukiwa mnyoofu, mwaminifu utasaidiwa na kila MTU,utawekwa juu
ya Mali nyingi na watu wengi (utawaongoza VIZURI).
Mwanzo 41:37-44 “Neno hilo likawa jema machoni pa Farao na
machoni pa watumishi wake wote. Farao
akawaambia watumishi wake: “Farao akawaambia watumwa wake, Tupate wapi mtu
mwingine kama huyu mwenye Roho wa Mungu ndani yake?. Farao akawaambia Yusufu
kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama
wewe. Basi wewe utakuwa juu ya nyumba yangu, na kwa neon lako watu wangu
watatawaliwa katika kiti cha enzi tu nitakuwa mkuu kuliko wewe. Farao
akawaambia Yusufu, tazama nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri. Farao akavua
pete yake ya muhuri mkononi mwake akaitia mkononi mwa Yusuph; akamvika mavazi
ya kitani nzuri na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni wake. Akampandisha katika
gari lake lile la pili alilokuwa nalo na watu wakapiga kelele mbele yake……”
Katika maisha unaweza kuwadanganya wengi sana, lakini huwezi
kuwadanganya hawa wawili yaani nafsi yako na Mungu wako. Ukiwa mnyoofu kwa hawa
wawili utapata mafanikio makubwa sana.
8. ONA UNACHOTAKA KUPITIA HICHO KIDOGO ULICHONACHO SASA.
-Kama unataka upate amani, furaha, upendo,afya n.k Ione
amani, furaha, upendo au afya hiyo NDANI ya moyo wako kwanza. Hivyo ndivyo
kupanda mbegu ya mafanikio kulivyo. Kama moyoni mwa mtu hakuna anachotaka,
atakipataje?
Tujifunze kwa Mama huyu katika 2Wafalme 4:1-6 “Basi mwanamke
mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha, akasema mtumishi
wako mme wangu amekufa; nawe wajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha BWANA; na
aliyemwia amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa. Elisha
akamwambia, nikufanyie nini?, Niambie; una kitu gani nyumbani.
Mungu akubariki sana
MAOMBI NA MAOMBEZI
MCHUNGAJI LAURENT MPOMA
0762756542
WATSAP: 0762756542
YOUTUBE: Upenyo Wa Mungu Tv
0 Comments