Follow us

SOMO: ZIJUE FAIDA ZA KUMTUMIKIA MUNGU

Tangazo

 


SOMO: ZIJUE FAIDA ZA KUMTUMIKIA MUNGU

“Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu”. Yohana 12:26

Kumtmikia Bwana ni nini?

 

Kumtumikia Mungu sio kuwa mchungaji, mwinjiristi, muhubili, mwimbaji, nabii, mtume n.k. bali kuna zaidi ya hapo. Kuna tafsiri mbalimbali za kibiblia zinazoelezea maana ya kumtumikia Mungu. Na baadhi ya maana hizo ni kama ifuatavyo;

 

1. Kumwabudu Mungu na kumsujudu yeye peke yake.

Ukiamua kumtumikia Mungu sio kuomba tu au kuhubili tu bali ni kumsujudia Mungu na kumwabudu yeye peke yake. Tunainama kwa Yesu peke yake na wala sio kwa watu, mizimu, waganga, mashetani n.k. bali tunainama kwa Yesu pekee.

“Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako”.Kutoka 23:25

 

”Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako”. Isaya 43:4

 

“Yesu akamjibu, Imeandikwa ya kwamba mtu hataishi kwa mkate tu. Akampandisha juu, akamwonyesha milki zote za ulimwengu kwa dakika moja. Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo”. Luka 4:4-6

 

2. Kumtii na kumtegemea yeye pekee.

Maana nyingine ya kumtumikia Mungu ni kumtii na kumtegemea yeye pekee, ukimfanya mwanadamu kuwa tegemeo lako na moyoni mwako umemwacha Mungu basi ujue kwamba umeliwa. Haimaanishi kwamba usitegemee msaada kutoka kwa mtu hapana bali unatakiwa kumtegemea Mungu moyoni mwako, kumtii yeye pekee kisha Yeye anatoa watu kwa ajili yako. Kama mtu hana tegemeo lingine utamwona kanisani masaa yote yaani Mungu atakuwa ndio tegemeo lake lakini kama moyoni mwake hakuna Mungu basi utamwona anategemea fedha, kazi, elimu yake n.k. na moyoni mwake amemwacha Mungu.

 

“Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi”; Isaya 1: 19

 

3. Kuwa na bidii katika kufanya kazi za Mungu.

Kazi za Mungu zipo nyingi sana sio kuhubili pekee. Mungu alipomwumba mwanadamu alimpa kazi ya kufanya duniani, unapokuwa na bidii katika kuifanya kazi yake, ukikamata kanuni ya Mungu ambayo ni biblia na kuyafanya yale yaliyoagizwa humo basi unakuwa unamtumikia Mungu. Kwenye nchi kuna kitu kinaitwa ilani hii ni lazima iendane na katiba ya nchi na sisi katiba yetu ni neno la Mungu ambalo ndio sheria ya Mungu ndani ya katiba kuna maagizo ya Mungu ambayo tunatakiwa kuyafanya. Kuzishika sheria za Bwana na kuzifanyia kazi ni kumtumikia Bwana.

“Lakini mjibidiishe sana kuzifanya amri na sheria, ambazo Musa, mtumishi wa Bwana, aliwaamuru, kumpenda Bwana, Mungu wenu, na kwenenda katika njia zake zote, na kuzishika amri zake, na kushikamana na yeye, na kumtumikia kwa moyo wenu wote na nafsi yenu yote”. Yoshua 22:5

 

Ukiizishika sheria za Bwana na kuzitenda ndio utumishi huo haikuhitaji uwe mchungaji. Unapowaleta watu nyumbni mwa Bwana umewajari na kuitimiza sheria ya Bwana. Yesu alipokuja duniani hakufungua shule kwa ajili ya kuwafundisha watu, hakuja kufungua kituo kwa kulelea watoto yatima n.k. alikuja kuondoa mapepo na ndio maana akawaita theneshara akawapa amri juu ya pepo wabaya ili kwamba wawatoe, unapofanya kwa bidii kazi ya kumtumikia Bwana maana yake unaishika sheria ya Bwana na kuwaleta watu nyumbani mwa Bwana kwa jina la Yesu Kristo.

 

“Palikuwa na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitalia, mtu mtauwa, mchaji wa Mungu, yeye na nyumba yake yote, naye alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu daima. Akaona katika maono waziwazi, kama saa tisa ya mchana, malaika wa Mungu, akimjia na kumwambia, Kornelio! Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Sala zako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu…….” Matendo 10:1-37

 

 

FAIDA ZA KUMTUMIKIA BWANA.

1. Kuokolewa kutoka gerezani ki muujiza.

“Akaondoka Kuhani Mkuu na wote waliokuwa pamoja naye, (hao ndio walio wa madhehebu ya Masadukayo), wamejaa wivu, wakawakamata mitume wakawaweka ndani ya gereza; lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema”, Matendo 5:17-19

 

Magereza yapo mengi sana yapo ya mateso, kukosa fedha, kukataliwa n.k. wanaokaa gerezani ni wafungwa na kufungwa ni kunyimwa uhuru wa kutenda. Mfungwa siku zote huwa anachaguliwa nini cha kula kwa kuwa anakuwa hana uwezo wa kuamua, unaweza ukawa kwenye kifungo cha uchumi yaani unakosa fedha hata ya kununua chakula. Leo hii ukiamua kumtumikia Mungu anakutoa kutoka kwenye gereza ulilo fungwa kwa jina la Yesu Kristo.

 

2. Kutoka kwenye mikono ya farao.

Kila mtu ana farao wa maisha yake, Farao ni ishara ya shetani anawakilisha shetani. Wana wa Israeli waliteseka sana wakatekwa na kuwekwa kwenye mikono ya farao, walikuwa watumwa miaka mia nne. Mungu alijua kwamba watu wale wanatakiwa kwenda kwenye nchi ya starehe yaani nchi ya ahadi lakini hatari yake ni kwamba walikuwa hawaendi. Kuna sehemu leo hii unahitaji kwenda lakini huendi kwa sababu ya farao wa maisha yako amekuzuia leo hii njia pekee ni kumtumikia Bwana.

“Kwa kuwa Bwana, Mungu wako, yuakuingiza katika nchi nzuri, nchi yenye vijito vya maji, na chemchemi, na visima, vibubujikavyo katika mabonde na milima”; Torati 8:7

 

Kuna mahali ni pazuri sana ambako unatakiwa kwenda, maisha yako yanatakiwa kuwa mazuri lakini leo hii huyaishi wala huyafikirii kwa sababu ya farao aliyekuzuia ili kwamba usiende. Nchi ambayo Bwana amekuaidia kuna mambo mengi mazuri ni mahali pazuri sana lakini farao amekuzuia kwa nguvu zote hataki kukuachia lakini faida ya kumtumikia Bwana ni kwamba Bwana akuondoa kwenye shida, mateso, akutoe kwenye mikono ya farao ili kwamba uishi maisha mazuri.

“Nawe umwambie Farao, Bwana asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu; nami nimekuambia, Mpe mwanangu ruhusa aende, ili apate kunitumikia, nawe umekataa kumpa ruhusa aende; angalia basi, mimi nitamwua mwanao, mzaliwa wa kwanza wako”. Kutoka 4:22-23

 

Mungu alimtuma Musa aende kwa farao ili kwamba amwambie awaache watu wa Mungu yaani wana wa Israeli ili kwamba waende wakamtumikie Bwana kanaani.

“Bwana akamwambia Musa, Ondoka asubuhi na mapema, ukasimame mbele ya Farao, umwambie, Bwana, Mungu wa Waebrania, asema, Wape watu wangu ruhusa waende ili wanitumikie”. Kutoka 9:13

 

3. Mungu atabariki chakula na maji

“Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako”. Kutoka 23:25

 

“Kwa hiyo Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, watumishi wangu watakula, bali ninyi mtaona njaa; tazama, watumishi wangu watakunywa, bali ninyi mtaona kiu; tazama, watumishi wangu watafurahi, bali ninyi mtatahayarika; tazama, watumishi wangu wataimba kwa furaha ya moyo, bali ninyi mtalia kwa huzuni ya moyo; mtapiga kelele kwa sababu ya uchungu wa roho zenu”. Isaya 65:13-14

 

4. Ukimtumikia Bwana anaondoa ugonjwa kati yako.

Kuna mambo mawili tofauti kuna uponyaji na kunakuondoa magonjwa. Ikiwa una malalia unapewa dawa ili kwamba zipambane na wale wadudu ndani yako sio kuondolewa ugonjwa. Ila ukiamua kumtumikia Bwana Mungu wako Mungu anaondoa ugonjwa ndani yako. Mkwe wake petro aliwahi kushikwa na homa na Yesu alipomwona na kumwombea akaondoa ule ugonjwa. Kuna magonjwa mengine hayajapona kwako ni kwa sababu hujaamua kumtumikia Bwana, leo hii amua kumtumikia Bwana kwa jina la Yesu Kristo.

Kuna mtu, joka, mchawi anakuwekea magonjwa lakini ukimtumikia Bwana Mungu anakuja na kuyaondoa magonjwa hayo wala hayatakuwepo kwako.

 

5. Hapata kuwa na mtu atakaye haribu mimba.

Ukimtumkia Mungu hapana kuharibu mimba kabisa, kuharibu mimba maana yake ni kuondokewa uhai, maana yake kitu kilikuwa hakijakomaa mpaka mwisho kinafia njiani. Inawezekana wewe ni mwanafunzi lakini kabla hujamaliza form four umepata ujauzito na kufukuzwa shule maana yake umeharibu mimba ya shule, unaweza kuwa unajambo zuri ambalo ulitakiwa ulizae lakini linaishia njiani. Umeenda kufuata nyanya ili kwamba upeleke dar es salaam kuuza ili upate faida unafika kitonga gari linapata ajari nyanya zile zinaharibika maan ayke umeharibu mimba ya biashara.

Bwana anasema kwamba ukimtumikia Bwana hutaharibu mimba, nyumba yako haitaishia njiani kwa jina la Yesu Kristo. Ukimtumikia Bwana hutaanza jambo na kuishia njiani kwa jina la Yesu Kristo

 

 

 

 

 

 

 

6. Hakuna utasa.

Ukimtumikia Mungu hakuna utasa, utasa ni ile hali ya kutozaa. Tumejifunza kwamba mwaka huu ni mwaka wa mavuno wachawi wanaweza kumzuia mtu asizae ili kwamba awe tasa, unajaribu kuongeza mitaji lakini haiongezeki kwa namna yeyote ile. Unaweza ukawa umechukua mtaji wako na kupanda shambani ili kwamba uvune mahindi mengi umewekeza milioni nne ili kwamba upate milioni kumi unashangaa mara ghafla jua limetoka huko na mvua imekataa mahindi yanakauka na baada ya kukauka mvua inanyesha lakini ukimtumikia Bwana Mungu ansaema kwamba hapata kuwa na tasa kwenye maisha yako.

 

7. Mungu atazitimiza siku zako.

Utimilifu wa siku ni kwamba kila mwanadamu unayemwona ana siku zake za ukamilifu. Kuna siku unatakiwa ufanikiwe hakuna kufa kabla ya wakati, hakuna kuanza jambo likaishia njiani ukiamua kumtumikia Bwana.

 

8. Mungu atawafanya adui zako wakukimbie.

Ukimtumikia Bwana yeye atasababisha adui zako wakimbie mbele zako

 

9. Mungu ataweka utiisho mbele yako

Ukimtumikia Bwana unaweza ukakaa na mawaziri lakini wakakuogopa na kusema mzee njoo na wakati huo wewe ni kijana kwa sababu ya kumtumikia Bwana. Kuna ndugu zako wanasema kwamba huyu ameokoka ametuasi tumuitishe aje kwenye kikao ama aache wokovu aingie kwenye ukoo au aendelee na wokovu tumtenge kwenye familia. Kama unamtumikia Yesu kwa ukweli ukifika kwenye kikao hicho wanasema kwamba tumekuita kwa sababu hatuja kuona siku nyingi tumekuita ili kwamba tukusalimie shauri lao linapotelea hapo.

Ukimtumika Bwana Mungu kuna utiisho anaweka mbele yako, bila utumishi wa Bwana ukitumikia fedha au mizimu utaangamia kabisa, leo hii amua kumtumikia Bwana kwa jina la Yesu Kristo.

 MUNGU AKUBARIKI

 

 

 

 


Post a Comment

0 Comments