Follow us

HATUA ZA KUSHINDA VITA VYA KIROHO KWA MAOMBI

Tangazo



HATUA ZA KUSHINDA VITA VYA KIROHO KWA MAOMBI

1.  Mtambue kwanza adui yako.

Waefeso 6:12 ”Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damuna nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.”

MAADUI TUNAOPAMBANA NAO NI HAWA.

-Falme za giza.

-Mamlaka za kishetani.

-Wakuu wa giza

-Majeshi ya pepo wabaya.

 2.  Tambua uwezo halisi wa adui yako.

Yakobo 4:7 ”Basi mtiini MUNGU. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.”

Adui yetu ni shetani na ana nguvu lakini taarifa ni kwamba tukimpinga na kumharibu kwa jina la YESU anaharibika.Katika vita yako ni muhimu kutambua uwezo wa adui yako.

3.  Tambua mbinu za adui yako.

2 Kor 2:11 ”Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake.”

-Mbinu za shetani ziko wazi sana kama wewe ni muombaji.Kupitia maombi utanoa macho yako ya rohoni ili yaone kila hila za adui dhidi yako hivyo utaomba kwa uhakika maana utakuwa unajua unapambana na nani na yuko wapi.

4.  Fahamu unapigana vita ya namna gani.

Siku zote ni muhimu sana kila mtu kujua kwamba vita ya kiroho hupiganwa rohoni.Kwenye vita hiyo ni lazima ujue kwamba ili ushinde vita unatakiwa uwe upande wa BWANA ndipo utashinda. Ili uwe upande wa MUNGU kwanza ni lazima uokoke na kisha ni lazima uongozwe na ROHO wa MUNGU. Ukishakubali kuongozwa na ROHO wa MUNGU basi hakika utajua Neno hili kwamba ”…..   BWANA awaambia hivi, Msiogope, wala msifadhaike kwa ajili ya jeshi kubwa hili; kwani vita si yenu bali ni ya MUNGU.2 Nyakati 20:15”

5.  Pima silaha zako, je zinauwezo wa kukufanya uanzishe vita?

Waefeso 6:13 ”Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za MUNGU, mpatekuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.”

 

Silaha za MUNGU ni;

 -Neno la MUNGU.

-Damu ya YESU.

-Jina la YESU.

-Matoleo.

-Matendo mema n.k

 Lakini silaha hizo haziwezi kutumika vyema kama wewe muombaji hutaomba kwa imani. Hivyo Imani ni risasi ndani ya silaha ya MUNGU hatakukuwezesha wewe kushinda vita ya kiroho,.

 6.  Pambana vita ya ushindi na sio vita ya kushindwa.

Vita ya ushindi inaanza kwanza kwa wewe mpiganani kuwa mtoto wa MUNGU  na kuongozwa na ROHO MTAKATIFU huku ukizijua  haki zako.

Warumi 8:14 ”Kwa kuwa wote wanaoongozwa na ROHO wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU.”

 Waebrania 11:6 ”Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye MUNGU lazima aamini kwamba yeye yuko, nakwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.”

 7. Tambua uwezo na Mamlaka iliyo upande wako.

1 Yohana 5:5 ”Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba YESU ni Mwanawa MUNGU?”

”Ninyi, watoto wadogo, mwatokana na MUNGU nanyi mmewashinda, kwasababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.-Yohana 4:4”

 

MUNGU AKUBARIKI SANA

MAOMBI NA MAOMBEZI

WASILIANA NA MCHUNGAJI LAURENT MPOMA

0762756542, 0782859946,

WATSAP: 0762756542


Post a Comment

0 Comments